MASWALI YA
VIKUNDI KF 120
1.
“Vipengele vya kibunilizi na utumiaji
wa wahusika katika kujadili dhamira kwenye kazi nyingi za fasihi andishi ya kiswahili umekuwa ukibadilika
toka enzi moja kwenda nyingine”. Muwe huru kutumia kazi zozote za kifasihi
kithibitisha ukweli wa hoja hiyo.
2.
“Shaaban Robert katika Adili na Nduguze amefanikiwa kujenga dhamira
zake kwa kutumia motifu ya safari”. Jadili.
3.
Huku ukirejelea mawazo na tafiti za
wataalamu mbalimbali jadili asili ya riwaya na mchango wa wajerumani kama
koloni katika maendeleo ya fasihi ya Kiswahili kihistoria.
4.
Huku ukirejelea mawazo na tafiti za
wataalamu mbalimbali jadili asili ya tamthilia na mchango wa Wakenya katika
kukua kwa tanzu hiyo.
5.
Huku ukirejelea mawazo na tafiti za
wataalamu mbalimbali jadili asili ya ushairi
na mchango wa wareno na waarabu katika kuenea kwa tanzu hiyo.
6.
Huku ukirejelea mawazo na tafiti za
wataalamu mbalimbali jadili asili ya ushairi na mchango wa wareno na waarabu
katika kukua kwa tanzu hiyo.
7.
Bainisha kwa mifano mchango wa Shaaban
Robert katika maendeleo ya fasihi andishi ya Kiswahili.
8.
Jadili jinsi Naratolojia katika Wasifu wa siti bint Saad unavyozipambanua
dhamira kirahisi ndani ya riwaya hiyo .
9.
Utomeleaji katika diwani ya Kiswahili na Malenga unaonekana kuwa na faida
na hasara katika kujadili dhamira kwenye diwani hiyo. Jadili.
10.
Wahusika katika riwaya za kingano wanamchango
gani katika kujadili dhamira za kazi ya fasihi kihistoria?
11.
Mgogoro wa mswahili ni nani unaathiri
vipi maendeleo ya fasihi ya Kiswahili hususani kwenye upande wa dhamira?
12.
Eleza mchango wa wataalamu wafuatao
katika kuibuka na kuendelea kwa riwaya ya Kiswahili:
·
Edward Steere
·
Carl Veltten
·
Edwin Brenn
·
Graham
Hyslop
13.
Jadili faida na hasara ya vipengele
vya kimajaribio katika kuchunguza dhamira kwenye kazi za fasihi ya kiswahili.
14.
Plato na Aristotle waliweka msingi
katika uundaji wa kazi za kisana. Jadili uzuri na ubaya wa misingi hiyo katika
kujadili dhamira ndani ya kazi za fasihi ya Kiswahili.
16.
Kujadili dhamira za kifasihi kistoria
kuna hasara kubwa zaidi ukilinganisha na faida nyingi tuzipatazo pindi
tunapojadili dhamira za kifasihi kwa mtindo mwingine. Tumia mifano lukuki
kueleza ukweli wa hoja hii.
17.
Riwaya ya Bwana Muyombekere na Bibi
Bugonoka ni miongoni mwa riwaya za Kiswahili za mwanzo kabisa. Jadili dhamira
na ufundi unaojitokeza katika riwaya hii.
18.
Maisha ni nini?
Wanafalsafa katika fasihi ya Kiswahili wanatoa majibu gani juu ya swali hili?.
Je,majibu yao yanakidhi matakwa ya kidhamira enzi hizi za sayansi na
teknolojia? Uwanja ni wenu kutoa mifano kun‘tu.
19.
Chunguzeni jinsi Epistemolojia katika
fasihi ya Kiswahili inavyokinzana kimaudhui kati ya enzi kabla ya uhuru na
baada ya uhuru.
20.
Miaka ya 1970 nadharia ya unegritudi ilitumika
sana kuhakiki dhamira katika kazi za kifasihi. Muwe huru kutumia mifano
mtakavyo kuthibitisha ukweli wa hoja hiyo.
21.
“Mlimbua
nchi ni Mwananchi.” Katika kujadili dhamira za fasihi ya Kiswahili kihistoria
methali hii imejipambanua vipi?
22.
“Vipera
vya semi vimetumiwa sana na waandishi wa fasihi ya Kiswahili katika kujadili
dhamira kihistoria.” Tumia Kiswahili
na Malenga na Haki ya Mtu
Haipotei kukanusha au kuunga mkono kauli hii.
23.
Huku
ukitumia mifano ya kazi za kifasihi, hakiki mabadiliko ya kihistoria kidhamira
katika vipindi vifuatavyo:
(a) Kabla ya ukoloni
(b) Wakati wa ukoloni
(c) Baada ya uhuru
24.
“Mashairi
ya Bongo Fleva nayo hayapo nyuma katika kudidimiza na kuibua historia mpya
ndani ya jamii ya Waswahili.” Hakiki kauli hii kwa kutumia wanamuziki wanne
ndani ya Afrika ya Mashariki.
.
Maswali yanatusaidia sana hususan mimi kama mwanafunzi chuo kikuu cha dar es salaam mlimani campus
ReplyDeleteMaswali yananifanya nielewe vitu vingi ahsante
ReplyDeleteNAOMBA UNIELEKEZE SWALI LA 8
ReplyDeleteTyunayasolve wenyew?
ReplyDeleteNzuri hiyo
ReplyDeleteIla mengine magumu
ReplyDeleteMaswali haya huongeza uelewa na kumfanya mwanafunzi asome kwabidii kukabiliana na mtihani wake, asante sana
ReplyDeleteMaswali haya huongeza uelewa na kumfanya mwanafunzi asome kwabidii kukabiliana na mtihani wake, asante sana
ReplyDeleteYanajenga akilii
ReplyDeleteUbarikiwe sana najivunia kua mwanafunzi wako.
ReplyDeleteAsante sana kwa kutusogezea maswali yenye kujenga uelewa
ReplyDeleteDaaah nimeyaona, by protee!UDOM coed @2020👍
ReplyDeleteNmeyaonaa piaa asante mwalimu wet u🤝
ReplyDeleteNa hii test ya kesho,baada ya kuona haya maswali i got scared
ReplyDeleteTunaomba na ufafanuzi
ReplyDeleteMbona hamtoi na ufafanuzi wa maswali haya
ReplyDeleteHakika kazi zako zimetukuka
ReplyDeleteHakika kazi zako zimetukuka
ReplyDeleteMaswali yako vizuri sana ila tatizo ni kupata marejeleo
ReplyDeleteMwl Mapunda umekua msaada mkubwa sana kwetu. Kazi yako ni tochi kwa mafinikio yetu haswa tunaosoma UDOM
ReplyDelete