UHAKIKI WA KIHISTORIA WA DHAMIRA ZA
FASIHI
KF 120
MANENO YANAYOJENGA MSINGI WA KOZI HII
NA UFAFANUZI WAKE;
- FASIHI
- DHAMIRA
- UHAKIKI
DHANA
YA NENO FASIHI
Mulokozi (2017) Anaeleza dhana ya
neno fasihi. Anasema “ Huko Ulaya Dhana ya neno fasihi imekuwa ikihusishwa na
neno la Kilatini Littera ambalo maana yake ya asili ni Herufi au Uandikaji.
Neno la kiingereza Literature limechipukia hapo.
KATIKA KULIZUNGUMZIA NENO
LITTERA/LITERATURE/UANDIKAJI, WANAZUONI
WANATOFAUTIANA KIMAWAZO. TOFAUTI HIZI TUNAZIITA MITAZAMO.
Mitazamo inayotawala dhana hii
ipo mitano (5) na dosari zake;
- Ni ule unaodai kuwa “Literature” ni jumla ya maandishi yote katika lugha fulani.
dosari
zake
(a) Mtazamo huu unapanua sana dhana ya
neno fasihi na kuingiza vitu ambavyo sio vya kifasihi.
(b) Mtazamo huu unaibagua fasihi
simulizi.
2. Mtazamo huu unadai kuwa
“Literature” ni maandiko bora. (Wasanii si watu wakawaida)
Dosari
(a) Mtazamo huu unaupa uzito
usanii na uwezo wa kubuni, lakini pia unaifinya fasihi kwa kuihusisha na
maandiko yaliyo bora tu.
3. Huu unadai kuwa “Literature”
ni sanaa ya lugha yenye ubunifu bila kujali kama imeandikwa au la. (Mtazamo huu
unahalalisha kuwa masimulizi ya kisanaa na nyimbo ni fasihi).
Mtazamo huu wa tatu ndio
unatawala hivi sasa katika taaluma ya fasihi ya Kiswahili. Inadaiwa kuwa neno
“fasihi” limetokana na neno “Fasuh” katika lugha ya Kiarabu lenye maana ya
“Ufasaha wa Lugha”
4. Mtazamo wa nne (4), ambao
ulizuka hapa Afrika Mashariki na kuenea sana miaka ya 1970 ni ule usemao kuwa
“Fasihi ni hisi….ambao zinajifafanua kwa njia ya lugha” (Ramadhani, J.A Mulika
2:6). Mtazamo huu unachanganya mambo matatu (3) ambayo ni (i) fasihi yenyewe
(ii) mambo yaelezwayo na fasihi (iii) mtindo wa kifasihi.
Dosari
Wenye mtazamo huu wamesahau kuwa,
mtindo wa kifasihi mara nyingi ni wa kifasihi, bali fasihi yenyewe si hisi.
Vivyo hivyo, fasihi huweza kueleza mapenzi, lakini fasihi yenyewe si mapenzi.
5. Mtazamo wa tano (5), ambao
hususan ni wa karne ya ishirini (20), ni ule ulioanzishwa na wafuasi wa
nadharia ya uumbuji (formalism). Mtazamo huu, ambao ulianzishwa na wanaisimu wa
Kirusi mwanzoni mwa karne ya 20. unadai kuwa fasihi ni tokeo la matumizi ya
lugha kwa njia isiyo ya kawaida ili kuleta athari maalumu. (wanamaanisha…
fasihi hukiuka taratibu za kawaida za matumizi ya lugha katika sarufi, maana na
sauti ili kumvutia na kumuathiri msikilizaji au msomaji).
Dosari
(a) Mtazamo huu umekosolewa kuwa
unaelemea mno upande wa fani na kupuuza maudhui, maana na muktadha wa kazi ya
fasihi.
(b) Mtazamo huu unasadifu zaidi
ushairi kuliko kumbo zingine za fasihi kama tamthiliya na riwaya ambazo si
lazima zitumie lugha kwa namna ya pekee.
MAANA YA FASIHI KWA MITAZAMO YA
UJUMLA……
Williady, (2015) Fasihi ni tawi
moja wapo la sanaa linalotumia lugha katika kuwasilisha ujumbe wa mdomo au wa
maandishi.
Wamitila (2004) Fasihi ni sanaa
inayotumia luha na ambayo hujishughulisha na binadamu pamoja na maisha yake na
huathri, hugusa au huacha athari fulanina hupatikana katika umbo ambalo
linatambuliwa na jamii Fulani.
Kwakuwa fasihi ni aina ya sanaa,
ni vyema mwanafunzi akajua pia maana ya sanaa.
MAANA YA SANAA
(Williady: 2015) Sanaa ni ujuzi
au ufundi wenye kuleta manufaa kwa umma.
AINA/ KUMBO/ TANZU ZA FASIHI
Katika tasnia ya fasihi na
taaluma zake kuna aina kuu mbili za fasihi, ambazo ni;
- Fasihi Simulizi
- Fasihi Andishi
UMBO LA SANAA
Tunaposema umbo la sanaa
tunamaanisha matawi yanayojenga sanaa. Matawi hayo nipamoja na;
Fasihi, maonyesho, ususi, uhunzi,
ufumaji, utarizi, uchongaji, ufinyanzi, uchoraji na muziki.
CHIMBUKO LA
FASIHI
Kuna nadharia kuu nne (4) za
chimbuko la fasihi na dosari zake;
1. Nadharia ya kidhanifu. Nadharia
hii inadai kuwa chimbuko la fasihi ni Mungu. Nadharia hii ni kongwe sana,
ilikuwa kabla ya Kristo. Nadharia hii ilianzia huko kwa Wayunani ambao
wanafahamika pia kama Wagiriki wa kale huko Ulaya. Hawa walikuwa na Miungu wa
ushairi na muziki waliowaita Muse, ambao yasemekana ndio
waliowapa watunzi muhu au kariha (msukumo wa
kiroho, kinafsi na kijaziba (inspiration) ) wa kutunga. Pia,
wanadai kuwa Mungu ndiye msanii mkuu. Kaumba ulimwengu kwa usanii wa ajabu.
Mwanadamu pia ni zao la sanaa ya Mungu. Hivyo uwezo wa mwanadamu wa kubuni
kampa Mungu, ambaye ndiye msanii mkuu.
DOSARI
§
Dosari
kuu ya nadharia hii ni kwamba inachanganya imani na taaluma (Ni nadharia isiyo
na uthibitisho au ushahidi kisayansi, hivyo ni ngumu kuijadili kitaaluma).
§
Pia,
nadharia hii inatafuta chimbuko la vitu vya kitamaduni nje ya maisha ya
mwanadamu na nje ya dunia hii.
2. Chimbuko la fasihi
ni “Sihiri”. “Sihiri” hapa inamaanisha uwezo au
nguvu ya kimiujiza inayotumiwa na watu kusababisha matokeo fulani. Katika lugha
ya kiingereza Sihiri huitwa Magic. Hawa
wanadai kuwa katika hatua ya awali katika maendeleo ya mwanadamu sayansi na
teknolojia vilikuwa katika hatua ya mwanzo kabisa. Hivyo Sihiri na
miujiza vilitumia nafasi ya sayansi, teknolojia na ugunduzi. Fasihi na sanaa
viliibuka kama chombo cha kuendeshea sihiri. Mfano wawindaji kabla ya
kwenda kuwinda waliichora picha kisha wakaichoma picha hiyo kwa mshale, tendo
hili lilimaanisha mavuno ya kutosha porini. Nyimbo walizoimba na maneno
waliyonuiza wakati wa kufanya sihiri hiyo ndiyo ushairi wa mwanzo.
DOSARI
§
Dosari ya
nadharia hii ni kwamba inachanganya dhima na chimbuko. Kutumika kwa sihiri
katika fasihi hakuthibitishi kuwa sihiri ndiyo chimbuko lake.
3. Fasihi imetokana na
mwigo(uigaji). Katika nadharia hii ambayo kwa lugha ya kiingereza inaitwa imitation,
na katika Kiyunani inaitwa mimesis, inaelezwa kuwa mwanadamu alianza
kuwa mbunifu kwa kuiga maumbile yaliyomzunguka, hivyo sanaa za mwanzo mara
nyingi zilijaribu kumathilisha vitu vilivyomo katika mazingira, kwa mfano
wanyama, ndege, miti, watu, na kadhalika.
DOSARI
§
Nadharia hii inasisitiza sana uigaji na kusahau
suala la ubunifu katika sanaa na fasihi. Pia, wamesahau kuwa ndani ya uigaji
kunavionjo vinavyotokana na ubunifu wa msanii.
4. Chimbuko la fasihi ni ile
hali ya kiyakinifu. Nadharia hii ambayo imejikita kwenye fikra za Marx na
Engels (rej. On Literature and Art, 1976) na nadharia ya ubadiliko (evolution)
ya Charles Darwin, hudai kuwa mwanadamu ni zao la maumbile asiliaya ulimwengu,
kuwa ubadilikaji wa taratibu wa mwanadamu kutoka katika hali ya unyama kuingia
katika hali ya utu umechukua mamilioni ya miaka, halikuwa tukio la siku au wiki
moja tu. Utamaduni, ikiwapo lugha na fasihi, ni zao la mabadiliko hayo.
.
DOSARI
Baadhi ya maelezo yahusuyo mabadiliko
ya mwanadamu kutoka katika usokwe kuingia katika utu,na hatua zake za mwanzo za
kujenga utamaduni na lugha, bado ni
mambo ya kidhahania ambayo hayajathibitishwa kwa ukamilifu.
Hata hivyo, nadharia ya kiyakinifu inaelekea
kukubalika zaidi kitaaluma kuliko nadharia zingine.
DHIMA ZA FASIHI
Fasihi hufanya kazi mbalimbali
katika maisha:
Kuelimisha jamii-Fasihi
hutumika kama nyenzo ya kuelimisha jamii, kupitia fasihi wanajamii wanaweza
kuelimishwa juu ya mambo mabalimbali, kama vile juu ya umuhimu wa kuishi kwa
amani, umuhimu wa kijikomboa kifikra, umuhimu wa kujikomboa kiuchumi, ubaya wa
ufisadi na kadhalika.
Kukuza utamaduni-Kupitia
fasihi simulizi, tamaduni na mila za jamii husika huhifadhiwa. Kwa mfano
kupitia methali, misemo, nahau na vitendawili unaweza kujua mila na tamaduni za
jamii husika.
Kukuza lugha-Fasihi
hutumia lugha kufikisha ujumbe wake katika jamii, lugha ya fasihi huwa ni ya
kisanaa zaidi na hivyo kuifanya iwe yenye mvuto kwa wasikilizaji au wasomaji.
Mtu anaposoma au kusikiliza kazi ya fasihi anapata ujuzi wa lugha. Lakini pia
fasihi yenyewe inaweza kutumika kama chombo cha kukuza lugha. Wasimulizi na
waandishi wa fasihi huhitaji kuwa na utajiri mkubwa wa lugha.
Kuburudisha jamii-Pamoja
na mambo mengine fasihi inalenga kuburudisha jamii. Kupitia takribani vipera
vyake vyote, fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua
hadhira, kwa mfano kupitia nyimbo, hadithi, mashairi na kadhalika.
Kukomboa jamii.
Kuonya jamii-Fasihi ina
jukumu la kuhakikisha wanajamii wanakaa katika mstari wa maadili ya jamii
husika. Kupitia fasihi wanajamii wanapewa mwongozo wa jinsi ya kufuata mwelekeo
unaokubalika katika jamii.
Kukuza uwezo wa kufikiri-Vipera
vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri sana ili kupata suluhisho. Kwa
mfano, vitendawili, ngano za mtanziko na kadhalika.
FASIHI YA KISWAHILI
Dhana ya “Fasihi ya Kiswahili” imekuwa
inawachanganya wanataaluma wengi. Hii kwa sababu inachanganya kwa pamoja dhana
kadhaa, ambazo ni:
§
Fasihi
ya Kiswahili
§
Fasihi
kwa Kiswahili
§
Fasihi ya Waswahili
Ili kuzielewa vema dhana hizo za fasihi ya
Kiswahili , kwanza tunatakiwa kumjua Mswahili.
Mswahili
ni nani?
Ponera (2010:69), Mswahili ni mtu mwenye
kiwango kikubwa cha umilisi wa lugha ya Kiswahili. Vilevile, ni mtu ambaye
amefungamana sana na mila na desturi za jamii ya watumiao lugha ya Kiswahili
kiasi hata cha kumuathiri kifikra, kimtazamo na kiitikadi.
FASIHI
YA MSWAHILI
Hii ni ile ambayo hutungwa
au kuandikwa kwa lugha ya
Kiswahili na Mswahili wa asili na fasihi hii hufuata mila na utamaduni wa
waswahili unaopatikana katika mazingira yake na hivyo humtambulisha mswahili.
SIFA
BAINIFU ZA FASIHI YA WASWAHILI
§
Hutungwa au kuandikwa na Mswahili wa asili.
§
Hutumia lugha ya Kiswahili.
§
Huakisi mila na desturi za Waswahili.
§
Nikitambulisho cha Mswahili.
§
Huwakilisha mtazamo na falsafa ya Mswahili
kuhusu maisha na ulimwengu.
FASIHI
YA KISWAHILI NI IPI?
Syambo na Mazrui (1992:ix) wanafafanua maana ya
Fasihi ya Kiswahili kuwa: .....hatuna budi kuichukulia Fasihi ya Kiswahili kuwa
ni ile iliyoandikwa kwa Kiswahili tu, iwapo inazungumzia utamaduni wa kiswahili
au utamaduni mwingineo. Maadamu fasihi hiyo imetumia lugha ya Kiswahili na
imefuata mbinu za ufasaha wa lugha hiyo, basi, kwa tafsiri yetu ni Fasihi ya
Kiswahili.
SIFA
BAINIFU ZA FASIHI YA KISWAHILI
§
Hutungwa au kuandikwa kwa Kiswahili.
§
Hutumia lugha ya Kiswahili.
§
Huakisi mila, utamdunina tajiriba ya mwananchi
wa Afrika ya Mashariki na Kati.
FASIHI KWA KISWAHILI
Mulokozi (2017), anasema, “Kuenea kwa Kiswahili
ndani na nje ya Afrika Mashariki, na hata nje ya bara la Afrika, na maingiliano
kati ya wazungumzaji wa Kiswahili na mataifa mengine, kumezua fungu la fasihi
ya kigeni katika lugha ya Kiswahili; kwa mfano tafsiri mbalimbali. Mifano
mizuri ni Biblia, Shakespeare Juliasi Kaizari, Kitereza (1980), hadithi
za Alfu Lela – Ulela, na kadhalika. Fasihi ya aina hiyo ndiyo tunayoiita
“Fasihi kwa Kiswahili” Hivyo “Fasihi kwa Kiswahili” ni tafsiri ya fasihi ya
mataifa mengine kwa lugha ya Kiswahili.
SIFA BAINIFU ZA FASIHI KWA KISWAHILI
- Ni fasihi iliyoandikwa kwa lugha nyingine isiyokuwa Kiswahili na kisha kufasiriwa kwa lugha ya Kiswahili.
- Huakisi mila, utamaduni na tajiriba ya kule ilikotoka, hivyo haimtambulishi Mswahili.
- Kwa kawaida huwakilisha mtazamo na falsafa ya jamii ya lugha chanzi.
AINA KUU ZA FASIHI YA KISWAHILI
Kuna aina kuu mbili (2) za fasihi ya kiswahili
ambazo ni:
Fasihi
Simulizi
2.
Fasihi Andishi
FASIHI SIMULIZI
Mulokozi (2017), anafafanua istilahi ya neno
“Simulizi” na mapungufu yake . Anasema “Fasihi simulizi ni istilahi inayotumiwa
kuelezea dhana ya fasihi itolewayo kwa mdomo bila kuandikwa. Istilahi hii, ambayo imezuka miaka ya 1970, ina
dosari, kwani neno “Simulizi” halina maana ya “Kitu kinachonenwa” (Kwa
Kiingereza: Oral) bali lina maana ya “Kitu kinachosimuliwa” (Kwa
Kiingereza : narrative). Hivyo tafsiri sahihi ya “Fasihi simulizi”
katika kiingereza ni “narrative Literature” siyo “Oral Literature”.
Hata hivyo kwa kuwa istilahi hiyo imekwishaenea na kukubalika, ni vigumu
kuibadili.
MAANA YA FASIHI SIMULIZI KWA UJUMLA......
Williady (2015) Fasihi simulizi
ni aina ya fasihi inayotumia mdomo na utendaji wa viungo vya mwili katika
kuwasilisha maudhui ya fanani kwa hadhira iliyokusudiwa.
TANZU ZA FASIHI SIMULIZI
Uainishaji wa tanzu za fasihi
simulizi bado unautata, wataalamu wengi wa taaluma za fasihi wanakinzana katika
kutoa idadi ya tanzu za fasihi na vipera vyake.
Balisidya (1987), anaainisha
“Mafungu” (kumbo/tanzu) tatu (3) za fasihi simulizi ambazo ni:
- Nathari
- Ushairi
- Semi
Balisidya, hakuishia kwenye
uainishaji wa tanzu tu, pia anaainisha na vipera vyake;
- Nathari
a)
Ngano
b)
Tarihi
c)
Visasili
2.
Ushari
a)
Nyimbo
b)
Maghani
3.
Semi
a)
Misemo
b)
Misimu
c)
Mafumbo
Nao TET (1976, 1988:120),
wanaainisha tanzu za fasihi simulizi na vipera vyake, kuwa ni:
1. Hadithi
(a) Ngano
(b) Tarihi
(c) Visasili
(d) Vigano
(e) Soga
2. Nudhumu/ushairi
(a) Ngonjera
(b) Maghani
(c) Nyimbo
(d) Ushairi
3. Semi
(a) Methali
(b) Misemo
(c)
Nahau
(d) Vitendawil
(e) Mizungu
M.M. Mulokozi (1996)
- Semi
(a) Methali
(b) Vitendawili
(c) Mafumbo
(d) lakabu
(e) Vitanzi – Ndimi
(f) Kauli - taulia
2. MAZUNGUMZO
(a) Hotuba
(b) Malumbano ya watani
(c) Ulumbi
(d) Mizaha
(e) Sala
3. MASIMULIZI/HADITHI
(a) Ngano
(b) Istiara
(c) Mbazi
(d) Michapo
(e) Hekaya
(f) Visasuli
(g) Visakale
(h) Mapisi
(i) Tarihi
(j) Nasabu
(k) Kumbukumbu
(l) Visasili vya ibada
(m) Visasili vya usuli
(n) Visasili vya miungu/ibada
4. MAIGIZO
(a) Maigizo ya watoto
(b) Maigizo ya sherehe
(c) Maigizo ya misiba
(d) Maigizo ya kidini
5. USHAIRI/NYIMBO
(a) Tumbuizo
(b) Tukuzo
(c) Chapuzi
(d) Tendi
6. USHAIRI / MAGHANI
(a) Ghani Nafsi
(b) Ghani Tumbuizi
(c) Ghani Sifo
(d) Ghani Masimulizi
7. NGOMEZI
(a) Ngomezi za Taarifa
(b) Ngomezi za Tahadhari
(c) Ngomezi za uhusiano (mf. Wa kimapenzi)
2. FASIHI ANDISHI
Hii ni aina ya Fasihi ambayo uwasilishaji wake
huwa kwa njiaya maandishi. Wataalamu wengi wa fasihi wanakubaliana kuwa fasihi
andishi imegawanyika katika tanzu kuu tatu (3) ambazo ni:
(i) Ushairi
(ii) Riwaya
(iii) Tamthiliya
Katika ngazi ya juu ya stadi za
fasihi andishi tanzu nyingine huongezeka, ambayo ni hadithi fupi.
MAANA YA USHAIRI
(WANA – MAPOKEO)
Shaaban Robert katika kitabu
chake cha “Kielezo cha Fasili” (1968:61) ana sema “Ushairi ni sanaa ya
vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi. Zaidi ya kuwa sanaa ya
vina, ushairi una ufasaha wa maneno machache au muhtasari. Mwauliza, shairi na
tenzi ni nini? Wimbo ni shairi dogo, ushairi ni wimbo mkubwa na tenzi ni upeo
wa ushairi. Mwauliza tena kina na ufasaha huweza kuwa nini? Kina ni mlingano wa
sauti za herufi. Kwa maneno mengine huitwa mizani ya sauti, na ufasaha ni uzuri
wa lugha. Mawazo maono na fikra za ndani zinapoelezwa kwa muhtasari wa shairi
huvuta moyo kwa namna ya ajabu”.
Udhaifu wa fasili hii
•
Udhaifu uliopo katika fasili hii ni kwamba,
ingawa ushairi wa aina yoyote unaweza kuimbwa, lakini siyo kila kiimbwacho
kitaitwa ushairi. Kwa mfano uimbaji wa hesabu kama vile wafanyavyo baadhi ya
walimu kuwakaririsha wanafunzi orodha ya kwanza mpaka kumi na mbili kwa hesabu za mara, huo si ushairi.
•
Sheikh Amri Abed Kaluta katika kitabu chake cha
“Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri” (1954:1) anafafanua maana
ya ushairi, anasema: ”Shairi au Utenzi ni wimbo, hivyo kama shairi haliimbiki
halina maana yoyote”
Udhaifu wa fasili hii
•
Udhaifu uliopo katika fasili hii ni kwamba,
Sheikh Amri Abed Kaluta amehusisha tanzu chache sana za ushairi katika fasili
yake yaani mashairi na tenzi na kusahau maghani, nyimbo na ngonjera.
Pia si lazima kila shairi
liimbike, yapo badhi ya mashairi ambayo hutolewa kwa kusemwa kama vile Maghani,
ambayo hughanwa.
(WANA-USASA)
M. Mulokozi na K. Kahigi katika “Kunga
za Ushairi na Lugha” (1982:25) wanasema “Ushairi ni sanaa inayopambanuliwa
kwa mpangilio maalum wa maneno fasaha na yenye muwala, kwa lugha ya mkato,
picha au sitiari au ishara, katika usemi, maandishi , au mahadhi ya wimbo, ili
kueleza wazo au mawazo, kufunza au kueleza tukio au hisi Fulani, kuhusu maisha
au mazingira ya binadamu, kwa njia inayogusa moyo”.
Masamba D.P. B (1983:59) anaeleza
kuwa “Ushairi ni utungo uliokusudia kueleza hisia za ndani alizonazo msemaji au
mshairi kwa kutumia lugha ya mkato au fupi, yenye mvuto kwa namna maneno
yanavyopangwa kwa kisanifu kwa uangalifu na ulinganifu, lugha yenye mvuto kwa
utamu wa maneno yake yenye mguso wa moyo kwa ajili ya mpangilio wa maneno
yake”.
VIPENGELE VYA USHAIRI WA
KISWAHILI
Ushairi wa Kiswahili unavipengele
vikuu viwili (2) Fani na Maudhui.
VIPENGELE VYA FANI
Hivi ni vipengele vya kiufundi
avitumiavyo msanii katika kuwasilisha ujumbe wa kazi yake kwa hadhira. Fani
huundwa na vipengele (vipera) vifuatavyo:
- WAHUSIKA
- MANDHARI
3. MUUNDO/UMBO (Vipande, Mshororo, Ubeti,
Vina na
Mizani)
3.
MATUMIZI YA LUGHA
2. RIWAYA
Nadharia ya Riwaya
Kumekuwa na misuguano kadhaa kutoka kwa
wanazuoni waliothubutu kutoa fasili ya riwaya. Imeonekana wazi kuwa
kunakukubaliana kwa baadhi ya masuala na kutofautiana pia katika kutoa fasili
hii. Miongoni mwa masuala yaliyopelekea misuguano katika utoaji wa fasili hii ni
pamoja na:
Dhima / maudhui ya riwaya
Mipaka ya riwaya pindi inapohusishwa
na hadithi fupi au novela
Ukubwa / urefu wa riwaya
Aina za riwaya
Kuna wengine huchanganya utanzu wa
riwaya na vijitanzu vingine vya kinathari (yaani, vile vitumiavyo lugha ya
mjazo) kama vile Hadithi fupi, Novela, Tawasifu na Wasifu.
Hadithi fupi
Tofauti yake na riwaya hujikita
katika upeo na uchangamani. Hii inamaana kuwa hadithi fupi huwa sahili sana
ilihali riwaya huwa imetanza zaidi.
Novela
Hii huwa ni changamani zaidi kuliko
hadithi fupi. Huweza kuwa na visa vingi kiasi kulinganisha na hadithi fupi.
Tawasifu
Ni utungo utumiao lugha ya mjazo
ukisimulia habari za mtunzi mwenyewe.
Wasifu
Ni utungo utumiao lugha ya mjazo
ambapo mtunzi husimulia habari za mtu mwingine.
Ukichunguza kwa makini vijitanzu
hivyo utaona kuwa vinatofautiana na riwaya katika vigezo vya: urefu,
uchangamani, idadi ya wahusika, lugha, vitushi, U―Kina, dhamira n.k.
Sifa bainifu za riwaya
Ilinganishwapo na tanzu nyingine,
riwaya huwa nasifa bainifu zifuatazo:
•
Kutokufungwa
na sheria nyingi (kinyume na makumbo mengine ya tamthiliya na ushairi).
•
Matumizi
ya lugha ya kinathari.
•
Kuwa
na mawanda mapana katika urefu na kina.
•
Ni
zao halisi la kibepari.
•
Kuwa
na uhalisi kwa kiasi kikubwa.
•
Mahitaji
ya kusoma na kuandika.
•
Kuwepo
kwa maisha na makazi yenye utulivu.
•
Kuwa
na uwezo wa kugusia hadi vitu vionekanavyo kama vidogo (kwa maelezo zaidi,
tazama. Madumulla, 2009).
TANZU ZA RIWAYA
Kwa kuzingatia vigezo vya maudhui, dhima na
mtindo, tanzu za riwaya ziko nyingi sana, ambazo ni:
(i)
Istiara
(Umbo la nje la riwaya hii ni kiwakilishi cha jambo jingine)
(ii)
Riwaya – barua
(iii)
Riwaya – chuku
(iv)
Riwaya – sira (Husimulia habari za maisha ya
mhusika tangu kuzaliwa)
(v)
Riwaya – tendi (Matendo ya ushujaa)
(vi)
Riwaya – teti (Ni riwaya inayosimulia vituko
na masaibu ya watu wapuuzi, walaghai, wajanja (maayari) )
(vii)
Riwaya – Jusura (Mikasa ya kussiimua damu)
(viii)
Riwaya ya Kifalsafa
(ix)
(ix)
Riwaya ya Kifanyakazi
(x)
(x) Riwaya ya Kihistoria
(xi)
(xi)
Riwaya ya Kijamii
(xii)
(xii)
Riwaya ya Kingano
(xiii)
(xiii)
Riwaya ya Kisaikolojia
(xiv)
(xiv)
Riwaya ya Kimahaba
(xv)
(xv)
Riwaya ya Kimajaribio
(xvi)
(xvi) Riwaya ya Ufungwa
(xvii)
(xvii)
Riwaya ya Uhalifu/Ujambazi
(xviii)
(xviii)
Riwaya ya Ujasusi
(xix)
(xix)
Riwaya ya Upelelezi
(xx)
(xx) Riwaya ya Utumwa/Simuluzi za Watumwa
(xxi)
(xxi) Riwaya ya Vita
(xxii)
(xxii)
Riwaya ya Vitisho
(xxiii)
(xxiii)
Riwaya ya Watoto
(xxiv)
(xxiv)
Riwaya ya Kisayansi
TAMTHILIA
Istilahi ya “Tamthilia” inatokana
na neno “Mithali” ambalo lina maana ya “mfano” au ishara ya kitu fulani. Hivyo
katika tamthilia kitu kimoja humathilishwa {ufananishwa} au huwakilishwa na
kitu kingine.
MAANA YA TAMTHILIA
Tamthilia au drama ni igizo la
kifasihi lililokusudiwa kutendwa jukwaani kwa ajili ya hadhira fulani. Hivyo,
kwa lugha ya kawaida, tamthilia huitwa mchezo wa kuigiza. Kwa kawaida tamthilia
huwa na masimulizi ambayo huigizwa na wahusika wa pande mbili au zaidi
zinazogongana. Mgongano huo hujenga mgogoro ambao unaposuluhishwa au kutatuliwa
mchezo huwa umemalizika.
TAMTHILIA NI SANAA ZA
MAONYESHO
Mlama (1983:203) anasema, sanaa
za maonyesho ni sanaa ambazo huwasilishwa, ana kwa ana, tukio fulani kwa
hadhira kwa kutumia usahii wa kiutendaji. Kwa mfano badala ya kuwasilisha wazo
kwa hadhira kwa kutumia maneno kama katika ushairi, sanaa za maonyesho huliweka
wazo lile katika hali ya tukio linaloweza kutendeka kwa kutumia usanii wa
utendaji kama vile vitendo, uchezaji ngoma n.k.
SIFA ZA TAMTHILIA /
SANAA ZA MAONYESHO
Muhando (Mlama) na Balisidya
(1976:4) wanatoa sifa (4) za sanaa za maonyesho;
1.
Dhana inayotendeka
2.
Mtendaji
3.
Uwanja wa kutendeka
4.
Watazamaji
Mulokozi
(2017) anatoa sifa (7);
1.
Dhana inayotendeka
2.
Uwanja wa kutendea
3.
Watendaji
4.
Hadhira
5.
Kusudio la kisanaa
6.
Muktadha wa kisanaa
Ubunifu
(Umathilishaji)
UHAKIKI
Uhakiki ni kitendo cha kusoma
kazi ya fasihi simulizi au andishi na kuchambua vipengele vya fani na maudhui
kwa kuangalia ubora na udhaifu wa kazi hiyo.
MHAKIKI NI
NANI?
Mhakiki ni yule mtu anayechambua
kazi ya fasihi, yaweza kuwa fasihi andishi au fasihi simulizi na kuchunguza
vipengele vya fani na maudhui.
DHIMA ZA
MHAKIKI
§
Kuchambua vipengele vya fani na maudhui.
§
Kueleza ubora na upungufu wa kazi hiyo.
§
Kueleza umuhimu wa kazi hiyo.
§
Kufafanua matumizi ya lugha ya picha, taswira na
mafumbo yaliyojitokeza katika kazi hiyo.
§
Kumshauri mwandishi juu ya maboresho ya kazi
yake.
VIPENGELE
VINAVYOFANYIWA UHAKIKI
Fani
§
Wahusika
§
Mtindo
§
Muundo
§
Mandhari
§
Matumizi ya lugha
Maudhui
§
Dhamira
§
Falsafa
§
Mtazamo/msimamo
§
Ujumbe
§
Migogoro
DHAMIRA
Tumeona kuwa
dhamira ni kipengele cha maudhui, hivyo ili kufaamu vizuri maana ya dhamira
tunatakiwa kujadili kwanza dhana ya maudhui.
Maudhui ni
nini?
§
Maudhui ni maana ya kazi ya fasihi au ni mawazo
yanayozungumzwa ndani ya kazi ya kifasihi.
§
Kwa kawaida; mwandishi hufafanua maana au
mawazo hayo kwa kupitia vipengele vyake
ambavyo ni dhamira, falsafa, mtazamo au msimamo, ujumbe na migogoro.
§
Wazo kuu
huitwa dhamira.
DHAMIRA
Dhamira ndio wazo kuu la mtunzi
katika kazi yake, linapotangamana na mtazamo wake hutupatia ujumbe auletao kwa
hadhira yake.
UHAKIKI WA KIHISTORIA
WA DHAMIRA ZA FASIHI YA KISWAHILI
Wataalamu katika taaluma za
fasihi ya kiswahili wanajadili historia na maendeleo ya fasihi ya kiswahili kwa
kugawa vipindi kadhaa tangu kuwako kwa kazi za kifasihi ulimwenguni. Katika
fasihi ya kiswahili wataalamu wanajadili vipindi vikuu tatu (3) ambavyo ni:
1.
Kipindi kabla ya ukoloni
2.
Kipindi cha ukoloni
3.
Kipindi baada ya uhuru
KIPINDI KABLA
YA UKOLONI
Miongoni mwa tanzu kuu tatu (3)
za fasihi ya Kiswahili, ushairi ndio tanzu ya kwanza kuwako kihistoria,
ikifuatiwa na riwaya na baadae tamthilia.
Tunapofuatilia historia ya
ushairi wa Kiswahili hatuna budi kuzingatia mambo mawili ya msingi:
Kwanza, ushairi simulizi
ulianza pale mwanadamu alipoanza kutumia lugha.
Pili, historia ya ushairi
andishi wa Kiswahili inahusishwa na ujio wa wageni katika Pwani ya Afrika
Mashariki. Hususani Waarabu ambao walileta hati ya Kiarabu na baadaye watu wa
Ulaya ambao walileta hati za Kirumi.
MAENDELEO YA FASIHI YA
KISWAHILI KIPINDI KABLA YA UKOLONI (Miaka ya 1000 hadi 1500 BK)
Kipindi kabla ya ukoloni ni
kipindi ambacho miji mingi ya Waafrika ilikuwa ikistawi polepole sana. Kipindi
hicho ushairi na kazi zingine za kifasihi zilipewa jukumu zito sana katika
jamii.
JUKUMU LA USHAIRI
KIPINDI HIKI
Ushairi ulikuwa na jukumu la
kuelimisha, kuonya, kuelekeza, kulea, kuburudisha n.k. Majukumu haya ya ushairi
yalikuwa ni kwa wanajamii wote kuanzia watoto wachanga hadi wazee, kuanzia uzima,
makuzi hadi kifo ushairi ulihusika. Mtoto alipozaliwa alipokelewa kwa nyimbo,
alipewa jina kwa nyimbo, akilia alibembelezwa kwa nyimbo, alijifunza vitu
mbalimbali vinavyozunguka mazingira yake kwa nyimbo, jando na unyago kwa
nyimbo, aliolewa au kuoa kwa nyimbo hadi kusindikizwa kaburini kwa nyimbo.
Nyimbo za wakati huo hazikuandikwa mahali
popote, na ushairi ulikuwa katika hali ya usimulizi. Maudhui yake yalihimiza
kazi na mambo fulanifulani katika jamii. Zipo tungo chache zilizohifadhiwa,
mfano Tungo za Fumo Liyongo. Fumo Liyongo alitunga tungo mbalimbali kama
vile Sifa za Mwana Munga, inasemekana utungo huu ulitungwa mwaka 1517.
Utungo huu ulihifadhiwa kichwani, kwa
sasa upo kama muswada. Wimbo huu ulimsifu mke wake, sifa za kuanzia kichwani
hadi nyayoni.
Utungo wa Hamziya ni
miongoni mwa tungo za kishairi za kale. Huu ni utungo wa kikasida unaomsifu
Mtume Mohammed, inasadikika kuwa ulitungwa mwaka 1652 au kabla ya hapo. Utungo
huu ni tafsiri ya utungo wa kiarabu Umma ul Qura (yaani mama wa mji) wa
mshairi wa ki – sufi kutoka Misri. Tungo zingine za zamani ni Utenzi wa
Tambuka (pia Chuo cha Herekali), Utenzi wa Vita vya Badri, Utendi
wa Ayubu, Utendi wa Mikidadi na Mayasa, Siri li – Asrari, Ayi
Wangiwangi, Utendi wa Qiyama, Kasida ya Burdai, Al – Inkishafi,
Shamiuni, Dua, Dura Mandhuma, Ukawafi wa Miraji, Utendi
wa Haudaji, Takhmisa ya Liyongo, Utenzi wa Shufaka n.k.
Kipindi hiki kilikwisha baada ya
uvamizi wa Waarabu katika miji ya Pwani ya Afrika ya Mashariki. Kumbuka kabla
ya Wareno tayari Waarabu walikuwa wana mahusiano mazuri na wenyeji wa miji ya
Pwani na miji mingine ya Pwani ilikuwa imestawi sana kwa sababu za kibiashara.
Ijapokuwa maandishi ya Kiarabu yalikuwepo lakini washairi wengi waliendelea
kutunga kwa ghibu kwa kuwa hayakukusudiwa kuhifadhiwa katika maandishi.
WAKATI WA WARENO (Miaka
ya 1500 hadi 1750)
Ikimbukwe kuwa katika miaka hii
ya 1500 hadi 1750 (Kipindi cha utawala wa wareno) kazi za kifasihi zilizotungwa
na kuandikwa bado zilikuwa ni zile za ushairi na tendi.
Historia inaeleza kuwa Wareno
waliingia Pwani ya Afrika ya Mashariki mwaka 1498. Kuingia kwao kulipigwa
vikali sana na wenyeji kwa kuwa walitaka kutumia mabavu kuhodhi biashara
iliyokuwa imeshamiri kati ya wenyeji na watu wa Bara la Asia. Kwa kuwa Wareno
walikuwa ni wafanyabiashara walitaka kumiliki bandari zote za miji ya Pwani ya
Afrika ya Mashariki.
Mwaka 1698 Ngome ya Wareno
iliangushwa rasmi na miaka ya 1728/30 Wareno walikuwa tayari wameondolewa Pwani
ya Afrika Mashariki. Kutokana na mapigano hayo miji mingi ya Afrika Mashariki
iliyokuwa imestawi kwa kiwango chake mfano Lamu na Pate
iliporomoka kabisa. Utenzi wa Al –Inkishafi unaelezea vizuri
anguko la miji hii. Hivyo kipindi cha Wareno hakikuwa na tungo nyingi, labda
kwa sababu tungi nyingi zilikuwa bado tungo simulizi. Hata hivyo zipo tungo
chache zilizotungwa kwa ajili ya kumpinga Mreno, ushairi wa mtunzi mwanamke
ulioitwa Mzungu Migeli, wake Mwana Mwinyi Mvita.
Katika moja ya
mabeti yake anasema:
Mzungu
Migeli umwongo,
Mato
yako yana tongo,
Kwani
kuata mpango,
Kwenda
kibanga uani (Hichens 1979:88).
Utungo mwingine
ni Portugezi Afala, Mmoja wa washairi alitongoa hivi:
Portugezi afala, faliki afala velo,
Baziiada sponyila watarafai biselo,
Si
nyama ya kuanila, defehati defehalo,
Vinyo
inakusumbula, vinyu na butizialo (Abdulazizi, 1979:90).
Kipindi hiki cha utawala wa
Wareno kazi za kifasihi zilizotawala katika ulingo wa fasihi ya kiswahili
zilikuwa ni ushairi tu na kwa kuwa hakukuwa na mabadiliko makubwa katika ushairi, hivyo hakukuwa na athari zozote za
kiarudhi zilizojitokeza.
WAKATI WA WAARABU (1750 – 1900)
Bado ushairi iliendelea kutamba
katika kipindi hiki.
Baada ya kufukuzwa Wareno,
Waomani nao hawakutaka kuondoka Pwani ya Afrika ya Mashariki, waliamua kukaa na
kutawala. Utawala wa Waarabu wa Omani ulipata nguvu zaidi kuanzia mwaka 1832.
Sultan Seyyid Said alipohamishia makao yake makuu katika kisiwa cha Zanzibar.
Waarabu kuanzia hapo wakafanya Pwani ya Afrka Mashariki kuwa koloni lao. Hapo
mapambano yakahamia kati ya Waswahili na Waarabu.
Kipindi hiki kilitawaliwa na
maisha ya Kimwinyi, Kibwanyenye na anasa nyingi. Ujio wa Waarabu ulileta athari
kubwa katika maendeleo ya ushairi (ikimbukwe kuw ushairi wa kiswahili kipindi
hiki ndio ilikuwa tanzu pekee katika fasihi
ya Kiswahili). Waarabu walileta dini ya Kiislamu na taaluma ya kuandika
kwa hati ya Kiarabu. Hivyo waswahili walishiriki katika utamaduni huo wa
Waarabu kwa kila namna, halikadhalika taaluma mbalimbali kwa kutumia lugha ya Kiarabu.
Wapo wenyeji walioslimu dini na wakajifunza kusoma na kuandika kiarabu kupitia
madrasa. Hivyo kusoma na kuandika kulienea sana miongoni mwa wale walioslimu.
Ukweli ni kwamba washairi wengi
wa ushairi wa Kiswahili wa mwanzo walikuwa ni Waislamu kwa sababu hiyo,
ijapokuwa hata ambao hawakuwa Waislamu wapo japo kwa idadi ndogo, waandishi
wengi walikuwa Mashekhe na walimu wa dini, hawa walijua hasa lugha ya kiarabu
na Korani tukufu.
Katika kipindi hiki kila Mswahili
aliyeishi maeneo haya alipenda chohote chenye uarabu, na uarabu ukawa ndio
kipimo cha ustaarabu.
Athari
zilizotokana na utawala wa Waarabu katika kazi za kifasihi (Ushairi) wa
Kiswahili
•
Athari za Kimsamiati na Kiistilahi
Lugha ya
Kiarabu ina maneno mengi katika ushairi hata katika lugha ya Kiswahili. Mfano
maneno kama alasiri, magharibi, darasa, kitabu n.k. Pia kuna istilahi
inazohusiana na ushairi tu, mfano shairi, tathmina, tathnia, tathlitha, tarbia
n.k.
•
Athari za Kimaudhui
Ushairi uliotungwa
kipindi cha Waarabu ulikuwa na maudhui yaliyogusa nyanja mbalimbali kama za
kisiasa, kidini, kibiashara na mahusiano ya kitabaka yaliyokuwepo.
Mfano kuwepo kwa upinzani kutoka
kwa Waswahili dhidi ya utawala kandamizi wa Waarabu kulichochea uandishi wa
mashairi mengi ya kisiasa, moja wapo ni Diwani ya Muyaka.
Muyaka alikuwa ni mwanasiasa
aliyetumia ushairi wake kupinga utawala wa Waarabu na alihimiza watu kuungana
ili kumng’oa Mwarabu. Utenzi wa Akida pia ulizungumzia harakati
za ukombozi dhidi ya Waarabu wa Omani.
•
Athari za Kiarudhi
Ushairi wa
Kiswahili uliathiriwa sana na taratibu za kiutunzi za Kiarabu. Mfano ushairi wa
Kiarabu ulisisitiza sana suala la utoshelevu wa kimaana katika mshororo na
ubeti. Hali hii pia tunaiona katika ushairi wa Kiswahili kwa wanamapokeo.
Ushairi wa kiarabu uligawa
mshororo vipande vikuu viwili, kwa kiarabu mgawanyo huu wa vipande uliitwa
misraa. Hata hivyo ushairi wa Kiswahili unavipande viwili na wakati mwingine
vitatu.
WAKATI WA UKOLONI WA
WADACHI NA WAJERUMANI (Miaka ya 1885 hadi 1910)
Kihistoria kipindi hiki kilikuwa
na upinzani mkali kati ya wenyeji na Wajerumani, hivyo kulikuwa na vita. Mfano
Mkwawa waliongoza majeshi yake kupigana na Wajerumani mwaka 1891 hadi 1898,
Abushiri na Bwana Heri 1888 hadi 1889, Isike wa Unyanyembe 1893, Mangi Meli wa
Moshi 1900 na Vita vya Majimaji 1905 hadi 1907.
Mbali na upinzani uliokuwepo,
wajerumani walisisitiza matumizi ya Kiswahili kwa watumishi wa serikalini na
Mashuleni na katika dini, mfano Biblia ilitafsiriwa katika lugha ya Kiswahili.
Magazeti mbalimbali yalianzishwa
katika kipindi hiki, kama vile Kiongozi (1905), habari za
Mwezi, Pwani na Bara, Baraza n.k. hivyo
mashairi mengi na hadithi fupi zilitungwa na kuchapishwa magazetini. Mashairi
na hadithi hizo ziliwapinga wakoloni, kazi hizo ziliandikwa kisitiari ili
kukwepa udhibiti. Mfano wa mashairi yaliyopinga ukoloni waziwazi enzi hizo ni
pamoja na Utenzi wa Vita vya Wadachi na Utenzi wa Vita vya
Majimaji. Pia mashairi na hadithi za kikasuku hazikukosekana. Wapo
baadhi ya waandishi waliotunga kwaajili ya kuwatukuza wakoloni na ukoloni. Hali
kadhalika kazi zingine za kifasihi zilizungumzia dhamira mbalimbali kama vile
mapenzi, kazi n.k.
Katika kipindi hiki ndipo sasa
riwaya ya kiswahili iliibuka.
KUIBUKA KWA RIWAYA YA KISWAHILI
Kuibuka kwa riwaya ya kiswahili kwa kiasi
kikubwa kumechangiwa na wageni (wakaloni na wamishenari). Katika kuibuka na makuzi yake riwaya ya
kiswahili imepitia hatua nne (4) muhimu. Hatua hizi nne zimeibuka ndani ya
utawala wa kijerumani pamoja na ule wa kiingereza ndani ya Afrika mashariki.
Kwanza, wageni (wakoloni na wamishenari) walikusanya
nathari za wenjeji.
Pili, ikafuata hatua ya kutafsiri ngano za wenyeji
katika lugha za kigeni. Kwa mfano, mwaka 1870 Edward Steere alianza kutafsiri
hadithi kutoka Zanzibar katika lugha ya Kiingereza. Mwaka 1889 alichapisha
kitabu kiitwacho Swahili Tales as Told by the Native of Zanzibar. Hiki
ni kitabu cha muhimu kwa sababu kinatoa dira kuhusu historia ya mwanzo ya
riwaya za Kiswahili. Mwaka 1907 Carl Vetten alichapisha kitabu kiitwacho Prosa
and Poesie de Suaheli kwa lugha ya kijerumani.
Tatu, ilikuwa ni kutafsiri fasihi za kigeni kuwa ya
Kiswahili. Kwa mfano, mwaka 1928 Edwin Brenn alitafsiri kitabu kiitwacho Alaza.
Mifano mingine ni: Alfu Lela Ulela, Mashimo ya Mfalme Suleimani, Hadithi
za Esopo, Hadithi za Mjoma Remas na Hekaya za Abunuasi. Kazi
hiyo ya kutafsiri ilipamba moto tangu mwaka 1930 wakati halmashauri ya
Kiswahili ya Afrika mashariki ilipoanzishwa.
Nne, waafrika kuanza kutunga riwaya. Walitunga
kutokana na kuhamasishwa na halmashauri hiyo ya Kiswahili. Mfano, mwaka 1934
James Mbotela alitunga riwaya ya Uhuru wa Watumwa. Riwaya hii
ilisanifiwa na Halmashauri ya Kiswahili kwa sababu iliwaponda Waarabu na
kuwakweza Waingereza ambao walikuwa katika Halmashauri ya Kiswahili.
Riwaya ya Uhuru wa Watumwa ni kielelezo
kimojawapo cha riwaya za mwanzo za Kiswahili. Watunzi wengine wa kiafrika ni
pamoja na Shaaban Robert na Abdallah S. Farsy (aliyetunga riwaya ya Kurwa na
Doto: 1961).
Baadhi ya waandishi wa kiafrika baada ya uhuru
walipanua wigo na kuandika juu ya mambo mengi zaidi. Mfano, zikatungwa riwaya
za upelelezi. Faraji katalambula alitunga riwaya ya Simu ya Kifo.
mohammed Said Abdallah alitunga riwaya nyingi za upelelezi mhusika wake mkuu
aliitwa MSA. Mifano ya kazi zake ni:
o
Duniani
Kuna watu
o
Kisima
cha Giningi
o
Mzimu
wa watu wa kale
o
Mwana
wa yungi Hulewa
o
Siri
ya sifuri
o
Kosa
la Bwana MSA
Kisha, watunzi wakageukia kutunga juu ya siasa
wakiongea juu ya masuala mbalimbali kama vile viongozi wanafiki, mikutano ya
siasa. Mifano ya kazi hizi ni: Njozi iliyopotea na Gamba la Nyoka.
Kwa ujumla, wanariwaya walikuwa wanaandika juu ya masuala ya jamii wakiwa na
nia ya kukosoa, kuelimisha na kadhalika. Waandishi wamekuwa wakikomaa katika
kuandika kwa kuzingatia maudhui na fani inayorandana na miktadha. Kabla ya
uhuru waliandika kikasuku pasipo kuchambua. Kwa mfano, Mbotela alipowasifia
waingereza katika Uhuru wa Watumwa. Pia uchoraji wa wahusika umekuwa
ukikomaa kutoka kipindi kimoja hadi kingine.
WAKATI WA UKOLONI WA
WAINGEREZA (Miaka ya 1919)
Kama ilivyokuwa wakati wa
Wajerumani, Waingereza nao walikikuza Kiswahili na kazi za kifasihi kupitia
elimu, dini, mashirika ya uchapishaji vitabu, kuendelezwa kwa hati ya Kirumi
n.k. vitabu vingi vilitungwa katika kipindi hiki vikiwemo vya somo la Kiswahili
sanifu na fasihi. Vitabu vingine vilitungwa ili kutoa maarifa mbalimbali kama
vile jinsi ya kutunga mashairi.
Baadala ya kutumia hati za
Kiarabu wakati huu zilitumika hati za Kiruni katika kuandika kazi za kifasihi,
wakati huo sanaa ilikuwa ni ya watu wa Pwani tu, lakini kipindi hiki ilienea
hadi ndani katika miji ya bara. Mfano Dodoma akina Mathias Mnyampala. Wakati
huo ushairi na kazi zingine za kifasihi zilikuwa zikitungwa na watu mbalimbali
tofauti na ilivyokuwa mwanzo ambapo watunzi walikuwa ni Waislamu tu
.
Kwa upande wa ushairi……
Kipindi hiki mashairi yalikuwa yakihoji, yakipinga na kujiuliza kuhusu utawala
wa wazungu. Pia yalikuwepo yale yaliyomsifu Malkia Elizabeth. Mashairi ya
Saadan Kandoro ni mfano mzuri wa harakati za kudai uhuru; kama yale ya Ondoka
Nchini Mwetu, Waafrika Njooni, Siafu Wamekazana, Kwetu ni
Kwao Kwanini? Mashairi haya yalikuwa ni ya kisiasa, pia yalikuwepo mengine
yaliyotaka uhuru wa kiutamaduni na uhuru wa kiuchumi. Mfano mashairi ya S.
Robert, Koja la Lugha na Pambo la Lugha.
Kanuni na taratibu za utunzi
hazikuathiriwa sana wakati wa Waingereza, ingawa wapo baadhi ya wanazuoni
wanaodai kuwa mashairi huru yalianza kipindi hiki cha utawala wa Waingereza.
Upande wa riwaya…. Wakati
wa mwingereza utanzu wa riwaya ulishaanza kukomaana, kazi nyingi za kinathari
zilishaandikwa. Kipindi hiki ndicho
kilikuwa kipindi cha kutamba kwa kazi za shaaban Robert. Riwaya ya Utubora
Mkulima ilitungwa miaka hii (yasemekana ilitungwa mwaka 1946).
Ikafuatiwa na riwaya ya Kufikirika 1947, Kusadikika
1951, Adili na Nduguze 1952 na Siku ya Watenzi Wote 1968.
Karibu riwaya zote za Shaaban Robert ziliathiriwa sana na ngano na hekaya, hasa
katika muundo wake na uchorajiwa wahusika (karibu wahusika wote wakuu ni bapa).
KUIBUKA KWA TAMTHILIA
Tamthilia za Kiswahili
zilizoandikwa kwanza kabla ya kuigizwa jukwaani zimeanza kutokea miaka ya 1950.
tamthilia za mwanzo zilikuwa ni za kidini. Kwa mfano, mwaka 1951 ilichapishwa
tamthilia ya C. Frank iliyoitwa Imekwisha. Tamthilia nyingiza
kidini ziliandikwa na kuigizwa tu shuleni na makanisani, lakini hazikuchapishwa
vitabuni.
Tamthilia za mwanzo zisizokuwa za
kidini zilianza kutungwa kati ya 1952 na 1956. shughuli za tamthilia wakati huo
wa “Hali ya Hatari” nchini Kenya zilisimamiwa na Graham Hyslop, mwingereza
aliyekuwa katika utumishi wa serikali ya kikoloni ya Kenya. Hyslop alianzisha
kikundi cha maigizo kwa ajili ya askari mwaka 1944, na miaka ya 1950 alianza
kutunga michezo ambayo iliigizwa na kikundi chake. Michezo yake ya mwanzo
katika lugha ya Kiswahili ni Afadhali Mchawi (EALB 1957) na Mgeni
Karibu (EALB 1957). michezo hiyo iliigizwa kati ya 1954 – 1956. Baadaye
Hyslop alianza kuzunguka katika shule na vyuo mbalimbali nchini Kenya
akifundisha muziki na uigizaji.
Miongoni mwa wanafunzi wa Hyslop
waliokuwa wakisoma Alliance High School, Nairobi, ni Henry Kuria, Kimani
Nyoike, Gerishon Ngugi na B.M. Kurutu. Tamthilia ya Kuria, Nampenda
Lakini… (EALB 1957) iliigizwa kwa mara ya kwanza 1954. tamthilia ya
Nyoike, Maisha ni Nini iliigizwa mwaka 1955. tamthilia ya
Gerishon Ngugi, Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi (EALB 1961) iliigizwa
mwaka 1956, na ya Kurutu, Atakiwa Polisi, mwaka 1957.
kwa jumla, hadi tunapata Uhuru,
tamthilia zote za Kiswahili zilizochapishwa zilikuwa zimeandikwa na Wakenya.
Watanzania hawakujitokeza katika uwanja huu hadi baada ya Uhuru.
Kipindi hiki pia kilikuwa ni
kipindi cha kudai uhuru. Dhamira za kupigania uhuru ziliandikwa kupitia vitabu
na magazeti ingawa kwa lugha ya kificho sana ili kukwepa udhibiti wa wakoloni.
Ni kipindi hiki ambapo harakati za kudai uhuru ziliendelea kupamba moto, wananchi
walizidi kupata mwamko wa kisiasa, kiutamaduni, mwamko wa Uafrika, kuanzishwa
vita vya MAUMAU, kuanzishwa kwa chama cha TANU, waandishi waliakisi mawazo
kutoka katika fukuto la kimapinduzi lililokuwepo katika jamii. Fasihi ilipata
nguvu kwa kuwa kulikuwa na vitu vingi vya kutolea hisia, mfano redio, magazeti,
vitabu n.k.
BAADA YA UHURU (Miaka
ya 1961 hadi 1970)
Baada ya kupata uhuru toka kwa
Waingereza watunzi wengi wa kazi za fasihi ya Kiswahili walisheherekea na
kushangilia hilo katika redio, magazeti na katika vitabu.
Kwenye ushairi. Dhamira
kuu ilikuwa ni masuala ya siasa. Mfano Saadan Kandoro katika Diwani ya
Saadani katika shairi la Nyerere Pokea Hicho (Yaani Kiti cha Uwaziri
Mkuu wa Tanganyika) uk. 145 na Tumshukuru Manani uk. 146 ni mfano wa
mashairi yaliyotungwa kipindi hiki ya kiwa na uwelekeo wa kisiasa. Pia zipo
baadhi ya Tenzi zilizotungwa kipindi hiki, mfano Utenzi wa Uhuru wa
Tanganyika (1967) uliotungwa na Mwinyi Khatibu Muhamed Amiri, Utenzi wa
Uhuru wa Kenya (1972) uliotungwa na Salum Kibao, Utenzi wa Jamhuri ya
Tanzania (1968) uliotungwa na Ramadhani Mwaruka n.k.
Kwenye Tamthilia. Baada ya Uhuru utunzi wa tamthilia ulipamba
moto zaidi, hasa upande wa Tanzania. Mashindano ya utunzi yaliendeshwa na Youth
Drama Association (Chama cha Drama cha Vijana) nchini Tanzania
yaliwawezesha watunzi chipukizi kujitokeza, mmoja wao akiwa ni Ebrahim Hussein
ambaye tamthilia yake ya kwanza, Wakati Ukuta (EAPH 1967)
ilishinda tunzo katika mashindano hayo. Wakati huo pia ndipo walipoanza kutokea
watunzi waliohitimu fani ya sanaa za maonesho katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam. Baadhi yao ni E. Hussein mwenyewe, Penina Muhando (Mlama), N. Ngahyoma,
G. Uhinga na E. Mbogo. Watunzi hao, hasa Hussein, Muhando na Mbogo, wametoka
mchango wa pekee katika maendeleo ya tamthilia ya Kiswahili
Kimaudhui, tunaweza
kuzigawa tamthilia za Kiswahili za 1960 – 2015 katika mikondo ifuatayo:
Migongano ya kitamaduni
Dhamira hii inajitokeza katika
umbo la mgongano wa utamaduni wa jadi wa Kiafrika na utamaduni wa Kizungu, au
katika mgongano kati ya mjini na shamba (tamthilia za vichekesho). Suala hili
limejadiliwa kwa kina zaidi katika baadhi ya tamthilia za Hussein (Wakati
Ukuta na Kwenye Ukingo wa Thim), Muhando Hatia
na Ngugi Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi…
Matatizo ya Kijamii na Kinafsi
(k.m. mapenzi, ndoa, ufukara, urithi n.k)
karibu tamthilia zote za mwanzo
zilihusu kipengele hiki. Kwa mfano Nakupenda Lakini… na Nimelogwa
Nisiwe na Mpenzi, zilizungumzia matatizo ya mapenzi yanayokumbana na
vikwazo vya kiuchumi au vinginevyo; na tamthilia za Hyslop zilihusu matatizo ya
urithi, rushwa, fitina na tamaa. Tatizo la mimba limejitokeza katika Hatia.
Katika Mke Mwenza tunakutana na tatizo la wivu katika muktadha wa
tatizo pana zaidi la ndoa za mitara, ambalo ni la kijinsia. Tamthilia ya
Semzaba ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe inalitazama suala la
mapenzi katika muktadha wa utumishi wa umma, na kuonesha kuwa mapenzi huweza
kuathri uwajibikaji kikazi. Katika Pambo (P. Muhando) suala la
elimu ya kishule na dhima yake katika maendeleo ya jamii linamulikwa. Pambo
mhusika mkuu, ni msomi wa chuo kikikuu ambaye anaoneshwa kuwa ana ‘Kichaa’ cha
kusaka pesa na raha badala ya kujinyima ili kuitumikia jamii. Inabidi jamii
nzima iingilie kati Kumrejesha katika njia inayofaa.
Dini.
Tamthilia zihusuzo dini zipo
katika makundi mawili.
Kwanza, ni kundi la
tamthilia za kanisani zenye kufundisha dini au kuadhimisha matukio ya kidini.
Tamthilia hizi, ambazo ziliigwa moja kwa moja kutoka Ulaya, hatutazizungumzia
hapa kwa vile hazihusishwi katika mijadala ya kifasihi.
Kundi la pili, ambalo
ndilo linatuhusu hapa, ni tamthilia zinazochambua na kuhakiki asasi na
mafundisho ya dini kifasihi.
Dini, kama asasi ya kijamii,
imejitokeza katika tamthilia kadha, hususan Topan Aliyeonja Pepo,
Muba Maalim, Mulokozi Mukwava wa Uhehe na Semzaba Tendehogo.
Kwa mfano katika Tendehogo, dini (Uislamu) inaoneshwa kama nyenzo ya kutengua
utu wa mtu wa mtumwa (Mwafrika) na kumdhibiti ili kumtawala.
Kwa upande wa dini ya asili
haijadiliwi sana katika tamthilia, na inapojadiliwa ama hubezwa, ama huoneshwa
kuwa ina nguvu na uwezo wa kuwaunganisha na kuwakomboa watu (mfano katika Kinjekitile
na Kija). Mara chache sana dini hiyo huoneshwa kuwa ni bora
kuliko dini za kigeni (kwa mfano katika H. Muhanika Njia Panda)
Matatizo ya kijinsia
Matatizo ya kijinsia, aghalabu
kwa mtazamo wa kifeministi, yanasawiriwa katika baadhi ya tamthilia. Watunzi
wanajaribu kuonesha hali duni ya mwanamke katika jamii ya sasa, kutafuta sababu
za hali hiyo, na kupendekeza ufumbuzi. Baadhi ya tamthilia zinazogusia suala
hili ni Muhando Nguzo Mama, Mulokozi Mukwava wa Uhehe,
Mazrui Kilio cha Haki, Hussein Kwenye Ukingo wa Thim na
Mbogo Tone la Mwisho.
Ukombozi wa taifa
Hili ni suala lililojitokeza
katika tamthilia nyingi. Baadhi ya watunzi wanaliangalia suala la ukombozi
katika muktadha wa ukoloni; wanasawiri harakati za upinzani dhidi ya ukoloni,
au ukombozi wa taifa. Mifano ni Nkera Mkwawa Mahinya na Johari
Ndogo, Hussein Kinjeketile, Mulokozi Mukwava wa
Uhehe, na Mbogo Tone la Mwisho.
Kwa ujumla, tamthilia hizi
zinauona ukombozi kama jambo la hakika ambalo haliepukiki, na haziishii katika
ukombozi wa kisiasa tu, bali zinaangalia pia ukombozi wa kiuchumi na
kitamaduni. Kuna uwezekano pia kuwa tamthilia ya kimafumbo ya Tambueni
Haki Zetu (P. Muhando) inasawiri dhana ya ukombozi wa taifa na utetezi
wa haki (ukiongozwa na Mundewa) dhidi ya kani za kitabaka na kijadi
zinazoukinza ukombozi huo.
Ujenzi wa jamii mpya
Hatua inayofuata baada ya
ukombozi wa kitaifa ni ujenzi wa jamii mpya. Hili ni suala ambalo
linawashughulisha watunzi wengi. Baadhi, kama N. Ngahyoma Kijiji Chetu na
M, Rutashobya Nuru Mpya, wanalitazama kimageuzi na kupendekeza
marekebisho katika mfumo uliopo, baadhi wanaonesha tu kuwa mambo siyo sawa,
kwamba ukombozi haujakamilika kwa vile mkoloni kabakia katika sura tofauti
(mfano Mbogo Giza Limeingia) na Hussein Mashetani,
na baadhi wanalitazama suala hili kitabaka na kuhimiza mapambano ya wafanyakazi
dhidi ya mabepari na ubepari (Kahigi na Ngemera Mwanzo wa Tufani na
Mazrui Kilio cha Haki.
Tamthilia za mwelekeo wa Thieta
ya Umma ambazo nyingi hazijachapishwa zinalitazama suala hili kwa mkabala wa
umma, kwa kuzingatia matatizo yao na mahitaji yao, siyo ya kitaifa tu, bali
hata ya pale walipo. Udikteta na ukandamizaji uliokithiri miaka ya ‘Uhuru’
katika nchi nyingi za Afrika unashambuliwa kisanaa katika tamthilia kadha.
Mfano mzuri ni tamthilia ya Kaptura la Marx (E. Kezilahabi)
inayoshutumu ukiritimba na matumizi mabaya ya madarak katika mfumo wa Ujamaa aliouanzisha
Raisi J.K. Nyerere nchini Tanzania. Mageuzi ya soko huria (utandawazi wa
kibepari) yaliyowageuza wanasiasa kuwa wafanyabiashara na baadhi kuwa mafisadi
yamesawiriwa katika tamthilia kadha pamoja na filamu za Kiswahili. Mfano ni
tamthilia ya F.P. Nyoni Mabepari wa Bongo.
Falsafa ya Maisha.
Tamthilia zenye kuzungumzia maisha kifalsafa, kama tunavyoona katika Utenzi
wa Inkishafi au katika riwaya za Kezilahabi bado hazijajitokza. Hata
hivyo, falsafa hugusiwa hapa na pale katika baadhi ya tamthilia, hasa zile za
Ebrahim Hussein. Kwa mfano, Kinjeketile haizungumzii suala la
vita vya ukombozi tu, bali pia inatupa tatizo la kifalsafa kuhusu nabii au
mkombozi anayeleta jambo ambalo linakua na kumzidi uwezo, na hivyo kumwangamiza
yeye na wafuasi wake. Kiistiara hapa tunaona usawiri wa nabii mkombozi (pengine
J.K. Nyerere au Kwame Nkrumah) anayeshindwa kufikia malengo yake. Kwenye
Ukingo wa Thim, pamoja na mambo mengine, inazungumzia falsafa ihusuyo
dhana za majaaliwa, bahati na malipo katika mazingira ya utamaduni wa Kiluo. Kija
ni tamthilia tata inayoibua falsafa ya Uafrika katika muktadha wa utandawazi.
Uchawi, Uganga na Itikadi za
Jadi
Masuala haya yanajitokeza katika
tamthilia kadha, mathalan Muhanika Njia Panda, Mbogo Ngoma
ya Ngw’anamalundi, Hussein Kinjeketile, Kitsao Mafarakano
na Kitogo Kija. Kwa jumla uganga na itikadi za jadi katika
tamthilia hizi zinasawiriwa kama amali muhimu za jamii zifaazo kutumiwa
kutanzulia baadhi ya matatizo ya kimaisha. Katika baadhi ya tamthilia za Thieta
ya Umma uchawi na itikadi za ushirikina zinaonyeshwa kama tatizo sugu lenye
kukwamisha maendeleo.
KUIBUKA KWA TAMTHILIA
ZA KIMAJARIBIO
Watunzi wengi wa tamthilia ya
Kiswahili wanaiga mbinu na kanuni za tamthilia ya Ulaya, hasa ya Ki –
Aristotle. Hivyo kisanaa tamthilia zao hazitofautiani na tamthilia za
Kiingereza, hasa za Kihalisia. Tofauti yao na watunzi wa Ulaya iko katika
maudhui na lugha iliyotumika tu. Watunzi wachache, kuanzia miaka ya 1970,
hawakuridhika na ukopaji huu; walihisi kuwa palihitajika tamthilia ya Kiafrika
yenye kuchota mbinu zake kutokana na sanaa za jadi za Kiafrika. Hiyo watunzi
hao walianzisha maigizo ya majaribio.
Miongoni mwa wana – majaribio hao
wa mwanzo ni Ebrahim Hussein. Mtunzi huyu alijaribu kutumia mbinu za utambaji
wa ngano katika maigizo yake ya Ngao ya Jadi na Jogoo
Kijijini. Mpaka sasa wataalamu hawajakubalia kama tungo hizo mbili
ziitwe tamthilia au tendi. Penina Muhando pia, katika tamthilia zake za Lia
Ubani na Nguzo Mama, vilevile alijaribu kutumia mbinu ya
utambaji wa ngano.
Majaribio ya kuifanya tamthilia
ioane na utamaduni na mazingira ya Kiafrika bado yanaendelea, na ni vigumu kwa
wakati huu kubashiri hatima yake itakuwaje. Yumkini kutokana na majaribio kama
haya tutapata aina ya tamthilia tunayoweza kuuita ya Kiafrika au ya Kiswahili
hasa.
KUIBUKA KWA THIETA YA
UMMA (POPULAR THEATRE)
Williady 2013, anaeleza maana ya
thieta ya umma. Anasema “Thieta ya Umma ni aina ya sanaa za maonyesho au
maigizo yaliyofanywa moja kwa moja jukwaani na wanajamii wa eneo fulani
wakishirikiana na wataalamu wa sanaa kwa lengo la kuyaibua, kuyaeleza na
kuyatolea suluhisho matatizo ya watu wa eneo husika.”
Muhando 1991,katika kitabu chake
kiitwacho Culture and development: The Popular Theatre Approach in Africa,
anaielezea vizuri dhana ya “Thieta ya Umma” au sanaa kwa maendeleo ya jamii.
Mhando anaitaja miaka ya 1970 kama nyakati za mwanzo katika vuguvugu la Thieta
ya Umma kwa nchi nyingi za Afrika. Majaribio kadhaa yalifanyika yaliyokuwa na
lengo la kuitambulisha dhana hii ya Thieta ya Umma kwa wanajamii. Kwa mfano
nchini Kenya dhana ya Thieta ya Umma ilijulikama sana kwa jina la “Thieta ya
Ukombozi”. Maigizo mengi ya namna hii yalizungumzia sana harakati za
ukombozi wa kifikra, kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa kwa mwafrika dhidi ya
utawala wa kikoloni.
Funzo kubwa tunalolipata kutokana
na vuguvugu la “Thieta ya Umma” ni kwamba watu wenyewe katika utamaduni wao
wanao uwezo na mbinu za kubuni drama zao wenyewe zenye kulingana na mahitaji na
matakwa ya kiujumi na kimaisha. Hivyo si lazima watunzi wetu wafuate kanuni za
Ki –Ulaya au Ki – Aristotle za utunzi wa tamthilia.
KUIBUKA KWA FILAMU YA
KISWAHILI
Mchepuo wa filamu katika drama ya
Kiswahili ulianza tangu miaka ya 1930 au kabla, wakati wakoloni walipoanza
kutengeneza na kuonesha filamu za Kiswahili, aghalabu zenye mafunzo kuhusu
masuala ya maendeleo kwa mfano afya, elimu, historia, sayansi kimu, na
kadhalika. Utaratibu huo uliendelea hadi miaka ya 1950 huku ukiratibiwa na
Idara za Ustawi wa Jamii. Nchini Tanzania Rashid Mfaume Kawawa, ambaye baadaye
alikuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais, alikuwa mwigizaji katika filamu hizo,
hususani filamu mashuhuri za mwanzoni mwa miaka ya 1950 za Muhogo Mchungu,
Meli Inakwenda na Chalo Amerudi. Wakati wa Ujamaa
Kampuni ya Filamu Tanzania (TFC) ilitengeneza filamu kadha, baadhi zikashadidia
sera ya nchi ya Ujamaa.
Tasnia ya filamu za Kiswahili
imekua zaidi miaka ya karibuni baada ya kuenea kwa televisheni, DVD na Video;
maigizo mengi ya tangu mwaka 1990 yanatumia vifaa hivyo. Katika miaka ya leo
filamu zimechukua nafasi ya tamthilia na kuwa ndiyo sanaa ya Umma ya maigizo
kwa Kiswahili.
Tasnia ya filamu ya “Bongo
Movies” inasemekana kuwa ya pili kwa ukubwa katika Afrika ikitanguliwa na
filamu za Kinaijeria.
RIWAYA BAADA YA UHURU
Baada ya uhuru riwaya ya Kiswahili imepiga hatua
kubwa sana. Umekuwepo mwondoko mpya katika maeneo kama vile ya:
§
Idadi ya kazi za riwaya
§
ubora wa riwaya zenyewe
§
Matumizi ya Lugha
§
mwelekeo wa maudhui
§
mabadilio ya motifu n.k.
Maendeleo haya ya ubunilizi wa
riwaya, pamoja na sababu nyingine, yamechochewa sana na ongezeko la hali ya
usomi na wasomaji katika jamii ya waswahili. Mchango wa ongezeko hilo la hali
ya usomi na wasomi katika jamii ya waswahili linaweza kutazamwa kupitia maeneo
kama vile; Utungaji, Usomi na utafiti kuhusu masuala ya riwaya.
AINA ZA RIWAYA
KWA KUZINGATIA MAUDHUI
Baada ya uhuru kulikuwa na ongezeko kubwa sana
la kazi za riwaya, hivyo pia tunaweza kuziweka riwaya kwenye makundi kwa
kutumia kigezo cha kimaudhui.
Riwaya za kihistoria
Riwaya za mwegamo huu huakisi matukio ya
kihistoria. Wahusika wake husawiri kwa makini ili kutia kumbukizi ya wakati
uliopita. Riwaya hizi si kitabu cha kihistoria, bali ni huakisi tu matukio ya
kihistoria. Huwa na urazini wa historia ya jamii. Mifano ya riwaya za mtazamo
huu ni: Miradi bubu ya Wazalendo (G. Ruhumbika), Kifo cha Ugenini (Olaf
Msewe), Kasri ya Mwinyi Fuadi (Shaffi Adam Shaffi), Zawadi ya Ushindi,
Kwa heri Islamagazi (Mapalala) na Moto wa Ngoma ya Mianzi
(Mulokozi).
Riwaya za Kimaadili (Riwaya za kidini)
Maranyingi hudokeza mapito ya mhusika mkuu toka
utoto wake. Hujaribu kueneza maadili kwa jamii. Wahusika huwekwa ili wawe
chachu ya maadili kwa jamii na kupinga uovu. Kwa mfano, Adili na nduguze
na Kusadikika vya Shaaban Robert. Aghalabu, hujikita katika masuala ya
dini. Misingi yake hukitwa katika vitu au mambo matatu ambayo ni:
Pathema (yaani makosa au kosa),
Mathema (yaani mafunzo au funzo) na
Catharsis (yaani utakaso).
Riwaya za Kiamapinduzi
Huwazindua wasomaji ili wapambane na udhalimu
na kubomoa mifumo ya ukandamizaji iliyopo katika jamii. Hudodosa dhana za
mapambano, mikinzano na matabaka, riwaya hizi maranyingi ni za kihalisia.
Mifano ya kazi za kundi hili ni: Kabwela (Abdulhaman Jumbe Safari), Ubeberu
Utashindwa (Kiimbika), Kuli na Haini (Shafi Adam Shafi), Kusadikika
(Shaaban Robert), Utengano (S.A. Mohamed na Dunia Mti Mkavu
(S.A. Mohamed).
Riwaya za Kisosholojia
Riwaya zake huchunguza na kuibua maswali ya
kijamii na kupiga darubini kali katika jamii. Hukazia vipengele vihusuvyo maisha
ya kila siku katika jamii (desturi, mila na mabadiliko ya jamii). Huwa na
uhalisi katika vipengele vyake. Maranyingi huwa na maudhui yenye kuhuwisha.
Hugusia migongano ya kijamii kama vile ukale na usasa, umji na uvijiji, familia
na ndoa kwa ujumla. Kwa mfano: Kurwa na Doto (M. Farsi), Dunia Uwanja
wa Fujo, Mzimu wa Babu ana Radhi (F. Nkwera), Bwana Mnyombekera
na Bibi Bugonoka na Harusi (A.J. Safari).
Riwaya za Kisaikolojia
Hujaribu kufichua hali ya kisaikolojia katika
jamii kwa kuwatumia baadhi ya wahusika. Maudhui yake huhusu vita vya mazoea
dhidi ya uhalisi. Hujadili mikinzano aipatayo mtu ki―nafsi, ki―jamii na
ki―uana. Hukitwa katika kuwako kwa (Kosa/udhaifu/jambo hasi/ utata na
misawajiko kwa mhusika kuu). Mfano: Tata
za Asumini (S. Ahmed) Kichwamaji (Kezlahabi).
Riwaya za Kifalsafa
Hujadili mambo yenye urazini fiche. Mtunzi
hudadisi mambo mbalimbali kwa jicho la kifalsafa (udodosi wa kina). Aghalabu,
hutumia lugha tata na ngumu. Miongoni mwa mambo hayo yanayododoswa ni kuishi,
ukweli, maisha, utu, kifo, kuwa na kutokuwapo kwa viumbe, kuwepo kwa Mungu n.k.
baadhi ya maswali ya kifalsafa yaulizwayo ni kama vile:
•
Maisha
ni nini?
•
Kuwapo
na kutokuwapo kwa dunia ni kwatokeaje?
•
Kuishi
ni nini?
•
Utu
ni nini?
•
Kwa
nini watu au vitu vipo hivyo vilivyo?
•
Kwa
nini mambo yapo hivyo yalivyo?
•
Mifano
ya riwaya za kifalsafa ni riwaya kadhaa za Kezilahabi. Nazo ni: Mzingile,
Nagona, Rosa Mistika, Kichwamaji. Riwaya za kifalsafa
zilizoandikwa na waandishi wengine ni pamoja na: Babu Alipofufuka, Umleavyo,
Walenisi, Mafuta na Bin―Adamu.
Riwaya Pendwa
Husisimua na huwa na mvuto wa pekee kwa
wasomaji. Aghalabu, fani hujichomoza zaidi kuliko maudhui. Pia humfikirisha
sana msomaji. Rejea sifa mbalimbali zilizojadiliwa katika tapo la riwaya pendwa
pamoja na mifano yake.
Riwaya za kitawasifu (riwaya sira)
Hizi ni tofauti na tawasifu. Riwaya zenye
mwegamo wa kitawasifu zimetungwa kama vile tawasifu. Tawasifu hueleza maisha ya
mtunzi. Riwaya ya kitawasifu hueleza maisha ya mhusika aliyeteuliwa na mtunzi.
Huweza kuegemea u―chanya tu na kuacha kudokeza mambo hasi. Hulenga kutoa
kumbukizi ili kuwahimiza wengine kuwa kama mhusika wa tawasifu. Katika riwaya
ya kitawasifu, sauti ya mtunzi husikika kupitia maisha ya mhusika. Mfano mzuri
wa tawasifu ni: Maisha yangu na baada ya Miaka Hamsini na Tippu Tip.
Riwaya za kiwasifu
Hizi hutungwa kama wasifu. Mtunzi hueleza
maisha ya wahusika fulani. Katika wasifu mwandishi hueleza juu ya mtu aliyewahi
kuishi au anayeishi. Wakati katika riwaya ya kiwasifu mtunzu hueleza maisha ya
kubuni ya mtu ambaye labda hajawahi kuishi. Mifano ya riwaya ya kiwasifu ni: Shida
(Ndyanoa Balisdya), Wasifu wa Siti Binti Saad (S. Robert), Salum
Addallah (J. Mkabarab), Maisha ya Seti Benjamini, Mtemi Mirambo
na Mkwawa na Kabila Lake.
KIPINDI CHA AZIMIO LA
ARUSHA
Azimio la Arusha lilileta sura na
dhamira mpya katika fasihi ya Kiswahili, watunzi wengi waliathiriwa na itikadi
hiyo ya siasa ya ujamaa na kujitegemea. Baadhi ya watunzi walitumiwa katika
kueneza na kufundisha siasa ya ujamaa na kujitegemea akiwemo Mathias Mnyampala
katika Ngonjera za Ukuta namba 1 na 2. Mashairi ya Azimio la Arusha (1971)
ambacho kilihaririwa na G. Kamenju na F. Topan. Baada ya kutangazwa azimio hilo
kazi za fasihi zilijitokeza katika sura tatu:
•
Fasihi ya Kindoto au Kinjozi
•
Fasihi ya kikasuku na
Fasihi ya
kitabiri
Fasihi ya
Kinjozi
Kazi za fasihi za Kinjozi ni
zile zilizosawiri matamanio ya Wananchi baada ya kutangazwa kwa Azimio la
Arusha kwamba wangekuwa na jamii mpya ambayo inajali haki na usawa wa binadamu.
Jamii inayoleta usawa na uhuru katika elimu, jamii inayopinga unyonyaji, jamii
inayopiga vita uzururaji na vijana kukimbilia mjini, jamii iliyoamini kwamba
vijiji vya ujamaa ndio suluhisho la matatizo yote ya kiuchumi, kisiasa na
kiutamaduni. Kazi kama riwaya ya Shida N.Balisidya, Ndoto ya Ndalia J.
Ngoma, Njozi za Usiku W. Seme na J. Mhina. Hii ni pamoja na Tamthilia za
Hatia, Dunia Iliyofarakana, Mwanzo wa Tufani, Kijiji Chetu
na Bwana Mkubwa.
Fasihi ya Kikasuku
Kazi za fasihi za Kikasuku ni
zile zilizoandikwa kwa kurudia yale yaliyosemwa na wanasiasa. Mwandishi anakuwa
kama kipaza sauti cha mwanasiasa, mwandishi hukosa muda wa kutulia na kuchambua
kwa kina kile kilichosemwa na wanasiasa. Kwa mfano katika Ngonjera za Ukuta namba
1 na 2. Mathias Mnyampala anakariri yote yaliyokuwa yakisemwa katika
kulitangaza Azimio la Arusha.
Fasihi ya
Kitabiri
Kazi za fasihi za Kitabiri huwa
katika namna ya kutabiri mambo mazuri ya wakati ujao, lakini hushindwa kuelezea
jitihada zipi zifanyike ili kufikia mafanikio hayo.
KIPINDI CHA MWAKA 1970
HADI 1980
Hiki ni kipindi kinacho husisha
miaka kumi baada ya Azimio la Arusha, kipindi hiki nacho kilikumbwa na mambo
mengi; kulikuwa na kuvamiwa na Dikteta Idd Amini. Kwa mfano Utenzi wa Vita
vya Kagera na Anguko la Idd Amini Dada (1981) uliotungwa na Henry Mhanika.
Katika kipindi hichi pia kulikuwa na ukosoaji wa mambo yanayojitokeza katika
utawala. Fasihi ilikuwa kwa namna ya kiuhakiki, mambo yalichunguzwa kwa undani
zaidi, hali ya kusifia sifia ilikoma. Kwa mfano riwaya ya Rosa Mistika (E.
Kezilahabi) iliihakiki jamii na kuwakosoa viongozi, Njozi iliyopotea
(C. Mng’ong’o), Njota ya Huzuni (Liwenga), Gamba la Nyoka (E.
Kezilahabi), kazi hizi zilionyesha matamanio na matarajio ya wananchi
kushindikana.
Baadaye ilijitokeza riwaya ya
kimapinduzi ambayo iliwahimiza wananchi kufanya mapinduzi ili kuondokana na
hali mbaya zilizopo. Ijapokuwa riwaya ya kimapinduzi ilisisitiza kupindua,
ilikuwa na ukasuku ndani yake. Kwa mfano Ubeberu Utashindwa,
Uzalendo, Kuli na Dunia Mti Mkavu. Palikuwepo na kitabu cha ushairi
kilichoitwa Miaka 10 baada ya Azimio la Arusha (1977) kilitolewa na
Ukuta na Mhariri alikuwa Abdullatif Abdalla.
Baada ya miaka kumi ya Azimio la
Arusha tamthilia nayo ilianza kugeuza mwelekeo wake. Badala ya kuusifu ujamaa kama ni ukombozi na
ujenzi wa jamii mpya tamthilia ikaanza kukosoa wanasiasa. Kati ya tamthilia za
aina hii ni Arusi, Nuru Mpya, Lina Ubani, Ayubu, Harakati za Ukombozi na
Mkokoteni. Nyingi kati ya tamthilia
hizi pia zilijitahidi kuondoka kwenye muundo wa uandikaji wa tamthiliya kama
ulivyopokelewa toka kwa wakoloni.
Tukumbuke kipindi hiki hali ya
uchumi haikuwa nzuri, kulikuwa na mambo ya ulanguzi, hivyo magazeti, vitabu
hata wanafasihi waliyaandika hayo. Hata hivyo waandishi makasuku waliosifia
viongozi waliendelea kuwapo. Wafuatao ni waandishi walioandika kazi zao katika
mkondo wa kiuhakiki:
Kwa upande wa ushairi kulikuwa
na; Euphrase Kezilahabi katika Kichoni na Karibu ndani (1988), M.
Mulokozi na K. Kahigi katika Malenga wa Bara (1976), Mohamed Seif
Khatibu katika Fungate ya Uhuru (1988) na Z. Mochiwa katika Mvumilivu
Hula Mbovu (1988). Washairi hawa wanawahimiza wananchi juu ya mambo fulani
fulani ya kufanya na wametoa mapendekezo yao. Wanataka ujenzi wa jamii mpya,
yaani pawepo na mabadiliko ya kiuchumi, kiutamaduni, kuwepo na haki, viongozi
kujirekebisha, uwepo wa usawa na utu na kuwepo na umoja. Kwa mfano katika Karibu
Ndani Kezilahabi katika shairi la Mkesha anaeleza uovu wa viongozi,
anawatanabaisha wananchi kuwa wanakesha wakati wengine wanakula.
Pia katika shairi la Sisi kwa
Sisi na la Hatumwoni kwamba kiongozi yupo tu kama kivuli hakuna
anachokifanya. Katika Fungate ya uhuru kuna Mashairi kama vile Haki,
Tumesalitiwa, Unganeni na Ningekuwa na Sauti.
Watunzi walionekana kana kwamba
wanadai uhuru tena kwa mara nyingine, hapa tunaweza kusema ni sawa na kunywea
chai ileile katika kikombe kipya. Dhamira ya siasa inaonekana kupewa nafasi
kubwa katika kujenga dhamira za watunzi.
Katika miaka ya 1980 ulijirudia kwa
nguvu mkondo wa riwaya pendwa, ambao ulijitokeza miaka ya 1960. Sababu za
riwaya pendwa kuibuka kwa nguvu katika kipindi hiki ni pamoja na Masuala ya
vita, matatizo ya kiuchumi na uhuru katika uchapishaji wa vitabu. Riwaya za
M.S. Abdulla ni Mzimu ya Watu wa Kale
(1960), Kisima cha Giningi(1968), Duniani kuna Watu(1973), Siri ya Sifuri (1974), Mke mmoja,
Waume watatu (1975), Mwana wa Yungi hulewa (1976) na Kosa la
Bwana Msa (1984).
Naye F. H. H Katalambulla
ameandika Simu ya Kifo. (1965), Pendo pevu (1976) Pilipili
(1977) na Unono (1978).
Musiba Aristablus Elvis akaandika
Kufa na Kupona (1974), Kikosi cha Kisasi (1979), (1980), Njama
(1981) na Hofu (1991).
Dhamira zilizoushughulisha mkondo
huu ni pamoja na mapenzi, upelelezi, ujambazi na ujasusi.
FASIHI KIPINDI CHA
MFUMO WA VYAMA VINGI
Mfumo wa vyama vingi nchini
Tanzania ulianza rasmi Julai mosi 1992. Uanzishwaji wa mfumo huo ulitokana na
mabadiliko ya kiulimwengu ya kisiasa, kufuatia kuanguka kwa dola la
Kisosholisti lililoongozwa na Urusi ambao ndio walikuwa na siasa za Usosholisti
(Ujamaa).
Kuanguka kwa dola hizi kulifanya
jumuiya za Ulaya mashariki kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi. Mabadiliko haya
ya Ulaya yaliungwa mkono na nguvu za Soko Huria ambapo wananchi walikuwa na
uwezo wa kuuza na kununua badala ya uchumi kuwa hodhi na serikali.
Mfumo huu unampa uhuru mtu yeyote
yule kujiunga na chama chochote cha kisiasa, hali kadhalika kwa kuzingatia
kanuni na sheria, mtu yeyote au kikundi cha watu wana haki ya kuanzisha chama
cha siasa.
Madhumuni ya uanzishwaji wa mfumo
huo ni kuimarisha demokrasia na kuwafanya watu waishi maisha bora.
MAFANIKIO
YANAYOTOKANA NA MFUMO WA VYAMA VINGI
•
Uhuru wa kutoa kero na kukosoa serikali.
•
Kufanya bunge kuwa chombo cha kuielekeza
serikali badala ya bunge kuelekezwa na chama.
•
Serikali
kukubali kukosolewa na kufanya marekebisho ili kukidhi matakwa ya wananchi.
•
Chama tawala kuwa tayari kukosolewa na kujikosoa
ili kiweze kuendelea kubaki madarakani.
MATATIZO
YATOKANAYO NA MFUMO HUU
•
Migogoro ndani ya vyama. Migogoro hii
husababishwa na harakati za kugombea uongozi na ruzuku.
•
Migogoro
ya chama na chama. Hii husababishwa na kutoridhika na utekelezaji wa sera
fulani au kupinga matokeo na kukosekana kwa uaminifu.
Kutokana na
mfumo huo, watunzi nao waliakisi hali hiyo katika kazi zao ingawa si kwa kiasi
kikubwa. Mfano T. mvungi katika “Mashairi ya Chekacheka”, shairi la “Taifa
wamelizika” uk. 2 beti 3 za mwisho. Anasisitiza umuhimu wa vyama vingi.
UHURU WA KUJIELEZA NA
KUKUA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kukua kwa vyombo vya habari na
uhuru wa kujieleza kumesaidia kuzuka na kuenea kwa kazi nyingi za kifasihi
ambazo zimekuwa na mchanganyiko wa dhamira kutokana na mfumo huu. Kazi hizi za
kifasihi mbali na kuburudisha, vilevile hubeba dhamira nzito zenye lengo la
kubadili mwenendo wa jamii husika. Mfano kipindi cha “Twende na wakati”
kilichokuwa kinarusha mubashara redio RTD (Redio Tanzania Dar es Salaam), “Orijino
Komedy” kilichokuwa kinarushwa TBC 1 na “Futuhi” kinachorushwa Star
TV.
Kukuwa kwa vyombo vya habari na
uhuru wa kujieleza pia hujitokeza kama dhamira mojawapo katika kipindi cha
vyama vingi. Suala hili kwa kiasi kikubwa linajitokeza katika Riwaya ya “Makuadi
wa Soko Huria” ya Chachage. Kupitia riwaya hii tunabaini kwamba, pamoja na
kuanzishwa kwa vyombo vingi vya habari lakini uhuru wa kujieleza wa waandishi
wa habari na wanafasihi kwa ujumla bado ni mdogo.
FASIHI YA KISWAHILI
KIPINDI CHA UTANDAWAZI
Utandawazi ni mchakato wa
kuunganisha uchumi, siasa na uhusiano wa kitamaduni wa mataifa mbalimbali
duniani
.
Utandawazi unaifanya dunia kuwa
kama kijiji kimoja kisichokuwa na mipaka. Mahusiano hayo ya jamii hupaliliwa na
maendeleo ya Sayansi na Teknolojia hasa kupitia sekta ya mawasiliano.
Utandawazi unasisitiza uondoaji
wa vikwazo vya biashara na kuifanya dunia kuwa soko moja. Kwa hiyo unahimiza
Soko Huria, Demokrasia, Utawala Bora, Usawa wa Kijinsia, Haki za Binadamu na
Utunzaji wa Mazingira miongoni mwa jamii husika.
ATHARI ZAKE KWA NCHI
MASKINI (ZINAZOENDELEA)
Athari zake nipamoja na kuongezeka
kwa hali ya umaskini, uchache wa vitegauchumi kwa wawekezaji,
kuendelea kukabiliwa na madeni,
hakuna ufanisi katika kilimo ambacho ndicho uti wa mgongo kwa kila nchi, uhaba
wa chakula na kuagiza kutoka nje, pamoja na maendeleo yote ya sayansi na teknolojia
rasilimali za nchi zinazidi kupungua thamani kutokana na tabia ya unyonyaji
inayofanywa na nchi tajiri kwa nchi masikini, kuibuka kwa mapigano ya wenyewe
kwa wenyewe yasababishwayo na uroho wa madaraka na tamaa ya kupata mali za
haraka haraka na kiwango kikubwa cha ujinga wa kutojua kusoma na kuandika.
KAZI ZA FASIHI ANDISHI
KIPINDI HIKI
Kipindi tunachoishi sasa ni
kipindi cha utandawazi wenye kushabihiana na kiwango kikubwa cha matumizi ya
Sayansi na Teknolojia.
Kipindi hiki kama ilivyo ada,
kazi za kifasihi hazipo nyuma katika kujadili masuala mbalimbali. Kazi nyingi
za kifasihi zinagawanyika katika makundi mawili.
Kundi la kwanza ni lile
linaloungamkono utandawazi na teknolojia.
Kundi la pili ni lile linalopinga
utandawazi na teknolojia ya hali ya juu kwa kuhofia kuporomoka kwa maadili yetu
ya Kiafrika.
Vilevile kazi nyingi za kifasihi
zinabeba dhamira zinazoshabihiana sana zikiongozwa na;
§
Mapenzi
§
Uongozi
mbaya
§
Usaliti
§
Siasa
§
Mila na
desturi
§
Ujenzi wa
jamii mpya
§
Rushwa
§
Matumizi
mabaya ya vyombo vya dola (jeshi)
§
Matabaka
Ebu tuchunguze
dhamira hizi ndani ya baadhi ya kazi za kifasihi zenye ladha ya utandawazi.
Makuadi wa
Soko Huria
Hii ni riwaya iliyoandikwa na
Chachage. Inatoa taswira ya mapambano dhidi ya ukoloni na baadaye dhidi ya
baadhi ya watu walioteka nyara uhuru wa wengi na kushirikiana na wageni kupora
rasilimali ya nchi kwa kisingizio cha sokohuria.
Riwaya hii pia inaweka bayana
uozo na udhalimu uliofichwa katika mfumo wa sokohuria, kama vile: Tamaa ya pesa,
ubinafsi na ukandamizaji, rushwa na utapeli.
Hata hivyo kwa upande mwingine,
riwaya hii inaleta matumaini kwa kuwa inaonesha watu wasivyokubali kukandamizwa
na wasivyokata tama katika kujitafutia haki zao.
Mwandishi anafikisha ujumbe
kupitia vipengele mbalimbali vya kifasihi kikiwemo cha wahusika.
Wahusika hao ni
kama vile:
Japhet
Lupacho
•
Kuadi na msaliti aliyeacha uzalendo na kukubali
kuvaa joho la ubaraka na ubarakala wa wawekezaji.
Mbunge Luhaba
•
Nikiwakilishi cha viongozi wa juu
wanaowakandamiza wananchi.
Binti Wenga
•
Anatetea haki za nchi hasa kupinga tabia ya
ubinasfi kwa viongozi.
Miraji na
Mrisho
•
Wazee wa rufiji wenyekupinga unyonyaji na
kutetea haki za wanyonge.
Wahusika wengine
ni pamoja na Janga Mjuba, Fidelis Mumi, Msakapanofu, Salama, Sifuni na Oscar
Mayowe
Msomi
Aliyebinafsishwa
Hii ni riwaya
iliyoandikwa na Nyambari Nyangwine mwaka 2012. Riwaya hii inazungumzia
matatatizo mbalimbali yanayoikumba jamii kutokana na suala la utandawazi.
Kikubwa ni ubinafsishaji na uwekezaji.
Wahusika
•
Mama Msagane
•
Entakana
•
Nyagichuro
Mabepari wa
Bongo
Hii ni tamthilia iliyoandikwa na
Frowin Paul Nyoni mwaka 2007. Nayo inazungumzia matatizo mbalimbali yaletwayo
na wachache hasa waliopewa dhamana ya uongozi. Suala la uwekezaji nalo
limejitokeza kwa kiasi kikubwa na athari zake pia zimeainishwa.
Wahusika
•
Mc Kilevi
•
Mke 1, 2, 3, 4
•
Mtoto 1, 2
•
Wawekezaji
•
Bibi Mtamba hadithi n.k
Wasakatonge
Hii ni diwani iliyoandikwa na
Muhammed Seif Khatib mwaka 2003. Inabainisha uozo ndani ya jamii na harufu ya
uozo huo inayoleta madhara makubwa kwa wanyonge. Ni sauti inayowatetea
wavujajasho ambao hudharauliwa na kuonewa. Na chanzo cha uozo wote huo ni huyuhuyu
anayeitwa utandawazi
be blessed
ReplyDeleteSina neno zaid ya safi sanaa
ReplyDeleteItakuwa vema Kama nikipata na kf 110 Asante kwa marifaa haya
ReplyDeleteVizur sana
ReplyDeleteNIMEFURAHISHWA NA DARASA HILI
ReplyDeleteSafi sana kazi nzuri
ReplyDeleteNi zaidi ya darasa. Ubarikiwe
ReplyDeleteBe blessed
ReplyDeleteBarikiwa nimejifunza kitu mwalimu wangu
ReplyDeleteOkay, iko poa
ReplyDeleteMie sina neno
ReplyDeleteUnajitole saana mwalimu Mungu akulipe kila la kheri!
Barikiwa
ReplyDeleteMungu akutie nguvu ktk kazi hii uzidi kupaa
ReplyDeleteSantee sana mungu akubalikia unatusaidia Sana
ReplyDeleteNimevutiwa sanaa asante mwalimu asante sanaa
ReplyDeleteAksante kwa matini haya, hakika nimepanua maarifa na upeo wa uelewa wangu juu ya fasihi.
ReplyDeleteHongera kwa kazi nzuri ya kuandaa wataalamu wa fasihi
God Bless u
ReplyDeleteUbarikiwe Dr kazi nzuri, tunakupenda sana.
ReplyDeleteMilele barikiwa sana mwalimu wetu fahari snaa kufundishwa na ww
ReplyDeleteMwalimu vizuri sana, vijana unatupa morali kwa kazi nzuri.
ReplyDeleteNapata maarifa adhimu ya fasihi yakiswahil
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteAsante mwalimu kwa maarifa, hakika, numejifunza mengi.
ReplyDeletePamoja sana mwalimu wetu kazi nzuri.Mungu azidi kukutia nguvu udumu katika ubora wako.
ReplyDeleteMwalimu ahsante kwa kazi yako nzuri
ReplyDeleteAhsante mwalimu kwa kazi nzuri
ReplyDeleteAsante Mr mungu akuzudishie sfya njema na mafuanikio
ReplyDeleteUbarikiwe sana mwalimu kwa kazi yako bora
ReplyDeleteTunaendelea kunufaika na kazi yako. Asante kwa maarifa haya.
ReplyDeleteGod bless you
ReplyDeleteAsante sana mwalimu
ReplyDeleteUmechimba vizuri ubarikiwe
ReplyDeleteOngera kwa kazi hiii
ReplyDeleteKazi nzuri ubarikiwe mwalimu
ReplyDeletePongezi ziwe na wewe sir unatupa vitu sahihi
ReplyDeleteMungu aendelee kukutia utashi kwa kazi nzuri uliyotoa kwa umma
ReplyDeletenini maana ya riwaya ya kisaikolojia kisaikolojia kama ilivyofasiliwa na wataalamu mbalimbali na misingi yake
ReplyDeleteMilele barikiwa mwalimu wetu mpendwa.
ReplyDeleteKazi nzur mwalimu wetuuu
ReplyDelete🙏🙏
ReplyDelete🙏🙏 iko vzr sana.
ReplyDeleteAs ant mwalim
ReplyDeleteAsante Sana mwl Mapunda zinatusaidia sana
ReplyDelete🙏🙏🙏🙏🙏
ReplyDeleteNzuri sana
ReplyDeleteNawapongeza sana kwa kazi hii nzuri kwani imesheheni ufafanuzi mzuri na wa kujitosheleza. Kutokana na makala hii, naomba kupewa ufafanuzi wa maneno mawili yafuatayo;
ReplyDelete1.Nostajia
2.Peojinasia
Ahsanten
Ubalikiwe sana mwalimu mwena!!
ReplyDeleteAsante sana ubarikiwe kwa kutusaidia katika hili
ReplyDeleteNzuri
ReplyDeletehttp://hmajumbeni.blogspot.com/p/blog-page_87.html?m=1
ReplyDeletehttps://www.coursehero.com/file/54042890/FASIHI-YA-KISWAHILIpptx/
ReplyDeleteNimejifunza kitu kikubwa sana kupitia ukurasa huu
ReplyDeleteMungu azidi kukutia nguvu kwa uweza wake
ReplyDeleteNimependezwa na darasa hili
ReplyDeleteNaomba msaada pia wa summary ya utangulizi wa isimu ya kiswahili
ReplyDeleteUmeiandika vzuri kwa uchambuzi mujaarabu lakni jarbu kutafiti juu ya thieta ya umma, pamoja na tamthiliya za kimajaribio
ReplyDeleteUbarikiwe saana umetatua changamoto nyingi
ReplyDeleteTunashukuru kwa msaada wako
ReplyDeleteKwa zaidi ya miaka 13 ya ndoa sikuweza kuzaa, naendelea kuharibika hata nikipata mimba, madaktari wote hawakuweza kunisaidia, hadi dada yangu akanielekeza kwa Dr DAWN, ambaye alinisaidia nikapata ujauzito na sasa hivi kuwa na mtoto mzuri wa kike,
ReplyDeleteAnasaidia pia marafiki zangu wengi niliowaelekeza, Dr DAWN ni baraka kwa kila mtu anayewasiliana naye,
*Kama unataka kupata mimba.
*Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
*Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
*Kama unataka mume/mkeo arudishwe.
*Kama unataka kurejesha mali yako iliyoibiwa au Pesa.
*Ukitaka kutibu aina yoyote ya ugonjwa,
Wasiliana naye kwa WhatsApp: +2349046229159